Marekani itaiwekea Sudan vikwazo vipya baada ya kubaini kuwa ilitumia silaha za kemikali mwaka jana katika vita vya wenyewe kwa …

Marekani itaiwekea Sudan vikwazo vipya baada ya kubaini kuwa ilitumia silaha za kemikali mwaka jana katika vita vya wenyewe kwa …

Marekani itaiwekea Sudan vikwazo vipya baada ya kubaini kuwa ilitumia silaha za kemikali mwaka jana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea dhidi ya Wanajeshi wa Rapid Support Forces (RSF), Wizara ya mambo ya nje imesema.

Usafirishaji wa bidhaa za Marekani kwa nchi hiyo utawekewa vikwazo na vikomo vya kukopa fedha kuwekwa kuanzia tarehe 6 Juni, taarifa kutoka kwa msemaji Tammy Bruce ilieleza.

Wanajeshi wa Sudan na kundi la wanamgambo la RSF hapo awali walishutumiwa kwa uhalifu wa kivita wakati wa vita.

BBC imewasiliana na Sudan ili kujibu hatua za hivi punde za Marekani. Maafisa wa Sudan wanasema bado hawana taarifa.

Zaidi ya watu 150,000 wameuawa wakati wa mzozo huo, ambao ulianza miaka miwili iliyopita wakati jeshi la Sudan na RSF walipoanza mapambano makali ya kuwania madaraka.

Katika miezi ya hivi karibuni, jeshi la Sudan limeuteka tena mji mkuu wa Khartoum, lakini mapigano yanaendelea kwingineko.

Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu silaha za kemikali ambazo Marekani ilisema ilizipata, lakini gazeti la New York Times liliripoti mwezi Januari kwamba Sudan ilitumia gesi ya klorini mara mbili, ambayo husababisha aina mbalimbali za madhara na hata vifo.

“Marekani inaitaka serikali ya Sudan kusitisha matumizi yote ya silaha za kemikali na kutekeleza wajibu wake chini ya CWC,” taarifa hiyo ilisomeka, ikirejelea Mkataba wa Silaha za Kemikali ambapo watia saini wamejitolea kuharibu hifadhi zao za silaha.

karibu katika kila nchi duniani, ikiwa ni pamoja na Sudan zimeukubali mkataba wa CWC, mbali na Misri, Korea Kaskazini na Sudan Kusini kulingana na Chama cha Kudhibiti Silaha, shiŕika la wanachama lisiloegemea upande wowote lenye makao yake makuu nchini Marekani.

“Marekani inasalia kujitolea kikamilifu kuwawajibisha wale wanaohusika na kuchangia kuenea kwa silaha za kemikali,” Bruce aliongeza.

#StarTvUpdate
#chanzobbcswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *