Marekani inapanga kufunga baadhi ya balozi zake barani Afrika

Marekani chini ya uongozi wa rais Donald Trump, inapanga kufunga baadhi ya Balozi zake katika mataifa ya Afrika, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Gazeti la The New York Times.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inapendekeza kufungwa kwa balozi za Marekani katika nchi sita ikiwemo  Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo Brazaville, Eritrea, Gambia, Lesotho na Sudan Kusini kuanzia tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka huu.

Ubalozi mdogo wa Marekani jijini Douala nchini Cameroon na Durban nchini Afrika Kusini, zimependekezwa pia kufungwa, ikiwa ni mkakati wa Washington kupunguza ushawishi wake wa kidiplomasia barani Afrika.

Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri wake wa mambo ya kigeni Marco Rubio
Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri wake wa mambo ya kigeni Marco Rubio REUTERS – Nathan Howard

Aidha, Ofisi maalum inayoshughulia masuala ya Afrika itafutwa na badala yake, kutakuwa na ofisi ya mjumbe maalum wa Afrika, ambayo itaripoti kwa Baraza la usalama la taifa kwenye Ikulu ya White House na sio Wizara ya Mambo ya nje.

Hata hivyo, ripoti ya mapendekezo haya yamekanushwa na Waziri wa Mambo ya nje Marco Rubio ambaye kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, amesema Gazeti la New York Times, limechapisha ripoti ya kupotosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *