Umoja wa Afrika, umeitaka nchi ya Marekani kufikiria upya uamuzi wake wa kupiga marufuku ya kuingia nchini humo kwa raia toka mataifa 12 duniani ikiwemo yale ya Afrika na Amerika.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wito wa AU umekuja saa chache tangu Rais Trump atangaze makataa hayo, aliyosema yamechochewa na tukio la hivi karibuni ambapo raia mmoja wa Misri aliwashambulia kwa moto waandamanaji wa Kiyahudi mjini Colorado.
Nchi za Afrika zilizolengwa katika makataa haya mapya ni pamoja na Chad, Congo Brazzaville, Equatorial Guinea, Libya, Eritrea, Somalia na Sudan.
Aidha Trump ameweka makataa ya muda ya kutoa viza kwa raia wa Burundi, Sierra Leone na Togo.

Mataifa mengine yaliyoguswa na hatua hii ya Trump ni pamoja na Afghanistan, Myanmar, Haiti, Iran, Venezuela, Cuba na Yemen.
Hata hivyo makataa haya hayatawahusu wanamichezo watakaoingia nchini humo kwa ajili ya fainali za kombe la dunia la mwakani pamoja na michezo ya Olimpiki ya Los Angeles ya mwaka 2028.
Makataa haya pia hayatawahusu wanadiplomasia toka kwenye mataifa tajwa.
Tayari tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa pamoja na shirika la Amnesty International; wamekosoa hatua hii ya Marekani waliyoitaja kuwa yakibaguzi na kinyume cha sheria za kimataifa.