Marekani: Hali ya wasiwasi yatanda Los Angeles baada ya siku tatu za makabiliano

Hali ya wasiwasi inaendelea kutanda Los Angeles siku ya Jumatatu, Juni 9, baada ya siku tatu za makabiliano wakati mwingine kati ya waandamanaji wanaopinga sera ya uhamiaji ya Donald Trump na vikosi vya usalama, huku rais wa Marekani akiwalaumu “wachochezi” kutoka makundi mbalimbali

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo yalianza siku ya Ijumaa, Juni 6, katika jiji kuu la California, ambako inaishi idadi kubwa ya Wahispania, wakati watu walijaribu kuingilia kati kukabiliana na kukamatwa kwa wahamiaji kwa nguvu na mamlaka ya uhamiaji yShirikisho (ICE).

Asubuhi ya Jumatatu, Juni 9, mabaki kadhaa ya magari yaliyochomwa moto siku moja kabla yalionekana kwenye barabara ya jiji, pamoja na jumbe nyingi zinazopinga ICE, polisi, na rais ziliandikwa kwa rangi kwenye majengo ya serikali. Polisi wa Los Angeles wanalindatoa ulinzi kwenye maeneo yenye watu wengi na kushika doria katikati mwa jiji, lililo tupu, ambalo lilitangazwa usiku kuwa eneo lililopigwa marufuku kwa maandamano au mikusanyiko kufuatia makabiliano ya siku moja iliopita.

Siku ya Jumatatu asubuhi, picha zilizopigwa kutoka angani zilizorushwa na kituo cha ABC7 pia zilionyesha mizozo kadhaa na makundi madogo waandamanaji. “Watu wanaosababisha matatizo ni wachochezi wa makundi mbalimbali na waasi,” rais wa Marekani amesema, bila kusema kama angetangaza hali ya uasi, ambayo ingempa mamlaka makubwa mno.

Meya wa Los Angeles, Karen Bass, kutoka chama cha Democratic amehakikisha kwamba makabiliano hayo yaliathiri tu “barabara chache” za katikati mwa jiji, na sio jiji zima, kinyume na kile Donald Trump amebainisha. “Watu waliochoma moto magari na kufanya vitendo vya uharibifu watachukuliwa hatua,” ameonya. “Hii haikubaliki.”

Donald Trump alijipongeza kwa kufanya “uamuzi bora” wa kupeleka walinzi wa taifa huko Los Angeles, mpango uliokosolewa na wanaharakati wa haki za kiraia na viongozi wa California, akiwemo gavana wake kutoka chama cha Democratic, Gavin Newsom. “Kama hatungefanya hivi, Los Angeles ingefutiwa kwenye ramani,” rais wa Marekani ametangaza kwenye mtandao wake wa Truh Social, akimshambulia tena gavana wa California kutoka chama cha Democratic, Gavin Newsom, na Meya wa Los Angeles, Karen Bass, ambaye aliwaona kuwa “hawafai kabisa.”

“Walichagua kudanganya wakazi wa California na Wamarekani kwa kusema hawakutuhitaji na kwa kuyaita ‘maandamano ya amani,” rais ameandika kwenye Truth Social. Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu uwezekano wa kukamatwa kwa gavana huyo wa California, mmoja wa wapenzi wake, Donald Trump amesema itakuwa “ni vyema.” “Alifanya kazi ya kutisha,” Donald Trump amebainisha.

“Rais wa Marekani ametoa wito wa kukamatwa kwa gavana aliye kazini. Hii ni siku ambayo nilitarajia sitawahi kuiona Marekani. Haijalishi wewe ni Mdemocrat au Mrepublican, huu ni mstari ambao hatuwezi kuuvuka kama taifa – hii ni hatua isiyoweza kukanushwa kuelekea ubabe,” gavana huyo wa California ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Rais “amesababisha vurugu na kutenda kinyume cha sheria kwa kuhamasisha walinzi wa kitaifa” bila kushauriana na mamlaka za mitaa-tukio la kwanza baada ya miaka sitini-amesema Gavin Newsom, ambaye ameahidi hatua za kisheria dhidi ya uamuzi huu.

Takriban askari 300 kati ya walinzi hawa wa kitaifa 2,000 , kikosi chenye silaha cha akiba mara nyingi kilikusanyika wakati wa majanga ya asili, kwa mfano, kiliwasilisiku ya Jumapili asubuhi. “Hatutaki kuona hali zaidi ya kijeshi,” Umoja wa Mataifa umesema Jumatatu.

Mamlaka ya Mexico imeeleza kuwa baadhi ya raia 40 wa Mexico walikamatwa Ijumaa na Jumamosi wakati wa operesheni kali za ICE, hali ambayo ilisababisha maandamano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *