Marekani: Donald Trump atangaza vita vya kibiashara duniani

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza Jumatano, Aprili 2, kwamba atatia saini agizo la utendaji linaloweka “ushuru wa kulipiza” kwa bidhaa zinazotoka nje za Marekani, katika kiwango sawa na zile zinazotozwa na washirika wa kibiashara wa Washington. Trump ametangaza ushuru mkubwa wa forodha wa 34% kwa China na 20% kwa Umoja wa Ulaya, EU. Kiwango cha chini cha ushuru wa forodha ni 10%.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Alikuwa akiitangaza kwa majuma kadhaa, na akatekelza hilo. Kwa Donald Trump, kile anachoita “Siku ya Ukombozi” ni moja ya siku muhimu zaidi katika historia ya Marekani. “Baada ya muda mchache, nitatia saini agieo la kihistoria la kuweka ushuru wa kuwiana kwa (uagizaji kutoka) nchi kote ulimwenguni,” Donald Trump amesema katika hotuba yake kutoka Ikulu ya White House. “Njia za kulipiza: kile wanachotufanyia, tunawafanyia. “Ni rahisi sana, haiwezi kuwa rahisi,” ameongeza rais wa Marekani, akisherehekea “moja ya siku muhimu zaidi katika historia ya Marekani.” 

Rais huyo kutoka chama cha Republican amezungumza juu ya “tangazo la uhuru wa kiuchumi” na kuahidi tena “zama za dhahabu” kwa nchi yake. “Kwa miongo kadhaa, nchi yetu imeporwa, kunyang’anywa, kufanyiwa madhila mbalimbali na kuharibiwa na mataifa ya karibu na ya mbali, washirika na maadui,” amesema. Ni zamu yetu ya kufanikiwa, na kwa kufanya hivyo, kutumia mabilioni na mabilioni ya dola ili kupunguza kodi zetu na kupunguza deni letu la taifa, na yote haya kwa haraka sana , amesisitiza kuwa mashambulizi ya Ikulu ya Marekani yamepangwa kama ifuatavyo: ushuru wa forodha wa chini wa 10% kwa bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje, ambazo huongezwa kwa malipo ya ziada kwa baadhi ya nchi zinazoonekana kuwa na uhasama hasa katika masuala ya biashara. Ada hizi za ziada zinakokotolewa ili kuakisi kile kinachoitwa vikwazo visivyo vya ushuru vilivyowekwa na nchi hizi wakati wa kuingia kwa bidhaa za Marekani, kwa mfano kanuni za afya na viwango vya mazingira.

Aidha, uagizaji kutoka China utatozwa ushuru wa asilimia 34%. Rais wa Marekani pia ametia saini agizo la kiutendaji kufuta msamaha wa ushuru wa forodha kwa vifurushi vidogo vilivyotumwa kutoka China, utaratibu ambao umeruhusu makampuni makubwa ya biashara ya mtandaoni ya China, Shein na Temu kujitanua nchini Marekani. Hadi sasa, imetoa ruhusa ya kutotozwa ushuru kwa usafirishaji wote ambao maudhui yake yalikuwa na thamani ya hadi dola 800.

Nchi za Ulaya zitatozwa ushuru wa 20%. Marekani itatoza ushuru wa 10% kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Uingereza. Bidhaa kutoka Japani na Korea Kusini huathiriwa na 24% na 25% mtawalia, au 46% kwa Vietnam. Rais wa Marekani pia ametangaza ushuru wa forodha wa 31% kwa Uswisi.

Kutokuwepo kwenye orodha: Mexico, Canada, Urusi … Orodha hiyo pia inajumuisha kutokuwepo kwa Mexico na Canada, ambazo zimekuwa zikilengwa hasa katika wiki za hivi karibuni, pamoja na Urusi.

Majirani wa Marekani, Canada na Mexico, zilizo chini ya makubaliano ya biashara huria (ACEUM au USMCA kwa Kiingereza), ziko chini ya sheria maalum. Bidhaa za Canada na Mexico ambazo zinatii masharti ya makubaliano kwa sasa hazitozwi kodi mpya. Kinyume chake, bidhaa zingine zinatozwa ushuru wa forodha hadi 25%.

Mataifa mengine ambayo tayari yamewekewa vikwazo (Belarus, Cuba, Korea Kaskazini, Urusi) hayajajumuishwa kwenye orodha kwa sababu hali hii tayari inazuia biashara zote muhimu na nchi hizi, kulingana na Ikulu ya White House. Ukraine inakabiliwa na ushuru wa forodha wa 10%.

Donald Trump amewataka viongozi wa kigeni kuondoa ushuru wao na kununua bidhaa zao. Ushuru mkubwa mpya uliozinduliwa na rais wa Marekani utaanza kutekelezwa Aprili 5 na 9, Ikulu ya White House imetangaza siku ya Jumatano.

Utekelezaji Ushuru mpya wa kuagiza uliozinduliwa na Donald Trump umepangwa kutekelezwa kwa awamu mbili, afisa wa Ikulu ya White amewaambia waandishi wa habari: Aprili 5 saa 12:01 asubuhi kwa saa za Ufaransa ushuru wa forodha wa angalau 10% kwa bidhaa zote zinazoingia Marekani, na Aprili 9 saa 12:01 asubuhi, kwa bidhaa zote zilizoongezwa ushuru wa forodha unaolenga mataifa makubwa kama China na Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent amezishauri “nchi zote wasilipize kisasi” dhidi ya ushuru wa serikali ya Trump, kwa kukabiliwa na “ongezeko la ushuru.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *