
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu ameagiza kusitishwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine huku kukiwa na mzozo kati ya Urusi, kufuatia mzozo wa Ijumaa ya wiki iliyopita na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Marekani Donald Trump ameagizwa kusitishwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine kufuatia mabishano ya siku ya Ijumaa na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, afisa wa Ikulu ya White House amesema siku ya Jumatatu jioni.
“Tunasitisha kwa muda na kukagua usaidizi wetu ili kuhakikisha kuwa unachangia suluhu,” afisa huyome, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, akisisitiza kwamba Marekani “inahitaji washirika wetu kujitolea kwa lengo” la amani.
Uamuzi huo umekuja baada ya mkutano katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu mchana na mkuu wa ulinzi Pete Hegseth na mkuu wa sera za kigeni Marco Rubio, pamoja na washauri wakuu wa Rais Donald Trump.
Uwasilishaji wa silaha umesitishwa
“Sio mwisho wa kudumu wa misaada, ni kusitishwa kwa muda,” afisa mwingine wa Marekani, pia akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina na kunukuliwa na kituo cha Fox News. Kulingana na Gazeri la Bloomberg, zana zote za kijeshi za Marekani ambazo bado hazijatumwa Ukraine “zimezuiwa,” ikiwa ni pamoja na silaha zinazosafirishwa kwa sasa na anga au baharini na silaha ambazo ziko katika maeneo ya usafiri nchini Poland.
Msaada wa kijeshi wa Marekani uliidhinishwa chini ya utawala wa awali wa Joe Biden. Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Marekani ilitoa “msaada wa kijeshi wa dola bilioni 65.9” kwa Ukraine kuanzia Februari 24, 2022 hadi Januari 20, 2025. Alipoulizwa kuhusu kuhusu suala hilo mapema siku ya Jumatatu, Donald Trump hakujibu wazi, lakini alionyesha kuwa majadiliano yalikuwa yakifanyika “tunapozungumza.” Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, alisema tena Zelensky anapaswa “kushukuru zaidi” kwa msaada wa Marekani.
Makamu wa Rais Amtuhumu Zelensky
Siku ya Jumatatu Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance alisema kwamba ana uhakika kwamba kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky hatimaye atakubali kujadili amani na Urusi, kufuatia mkanganyiko wa mkutano wake na Donald Trump siku ya Ijumaa. Katika mahojiano na Fox News, alisema rais wa Ukraine “ameonyesha kukataa wazi kushiriki katika mchakato wa amani” unaotakwa na rais wa Marekkani. “Nadhani Zelensky hhajakuwa tayari bado, na nadhani, kusema ukweli, bado hayupo tayari, lakini nadhani hatimaye atakubali. “Ni lazima,” makamu wa rais alisema katika mahojiano hayo, yaliyorekodiwa kabla ya tangazo la kusitishwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine.
Alipoulizwa ikiwa mlango wa Ikulu ya White House utabaki wazi, alijibu: “Rais Trump ameweka wazi na thabiti kwamba mlango uko wazi mradi Zelensky yuko tayari kuzungumza kwa umakini juu ya amani.” Lakini “huwezi kuja kwa Ofisi ya Oval au popote pengine na kukataa kujadili hata maelezo ya makubaliano ya amani,” alisema, akisisitiza kwamba Urusi na Ukraine zitalazimika kufanya makubaliano.
Makamu wa rais wa Marekani alizishambulia tena nchi za Ulaya, akizitaka kuwa “wa kweli”, akisema kuwa “vita hivi haviwezi kudumu kwa muda usiojulikana”.