Marekani: Donald Trump aahidi malipo ya ushuru wa forodha na mataifa mengine duniani

Nchini Marekani, Donald Trump anaanza tena mojawapo ya shughuli zake anazozipenda zaidi: kutoza ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani. Siku ya Alhamisi, Februari 13, alifungua mlango kwa kanuni ya usawa katika suala hilo.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Dakika chache kabla ya kumpokea Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Rais wa Marekani Donald Trump amehakikisha kwamba ataweka “ushuru wa forodha” ili kurejesha “haki” katika mahusiano ya kibiashara kati ya Marekani na dunia nzima, bila hata hivyo kutoa tarehe maalum ya mwisho. “Ikiwa watatuwekea ushuru au kodi, tunaweka kiwango sawa cha ushuru au kodi kwao pia, ni rahisi kama hivyo,” Donald Trump amesema kutoka Ikulu ya White House.

Serikali ya Marekani haijatoa makataa mahususi, ilhali tayari imeweka, tangu mwanzoni mwa muhula wa pili wa Donald Trump, asilimia 10 ya ushuru wa ziada wa forodha kwa bidhaa za China, na hivi karibuni asilimia 25 ya ushuru wa forodha kwa chuma na alumini kuingia Marekani.

Rais Donald Trump amekubali kwamba bei “zinaweza kuongezeka kwa muda mfupi” kwa kaya za Marekani, lakini amekadiria kuwa hatimaye zitapungua. Amebaini kwamba nchi nzima itanufaika na vikwazo hivyo vya forodha, ambavyo vinakusudiwa kuilinda vyema sekta hiyo dhidi ya ushindani na kupunguza nakisi ya biashara nchini, ambayo inazidi euro bilioni elfu moja (bila huduma).

Kanuni zinazoadhibu bidhaa za Marekani pia vinalengwa na Donald Trump

Lakini serikali ya Marekani hataki kuishia hapo: pia inalenga vikwazo visivyo vya desturi kama vile kanuni za kuadhibu bidhaa za Marekani, au VAT ambayo mataifa hukusanya kwa kila ununuzi. Ujerumani, kwa mfano, inatoza ushuru wa 19% kwa bidhaa zote zinazouzwa nchini – Ujerumani na nje.

Utaratibu huo unaelezewa na Donald Trump kuwa “wa kuadhibu”, kwa sababu unajumuishwa na ushuru wa forodha wakati wa kuingia nchini. Washirika wa Marekani “mara nyingi wana tabia ndogo kuliko maadui zetu” kwenye biashara, mkuu wa nchi amesema, akitaja tabia ya Umoja wa Ulaya kuhusu biashara kuwa “kali zaidi.”

Kwa mara nyingine tena, anatishia Umoja wa Ulaya, ambao anautuhumu kuchukua fursa ya Marekani. Kama zile za awali za Canada au Mexico, ada hizi hazitatumika mara moja. Itachukua muda kwa huduma zake kutathmini ni kiasi gani cha ushuru wa forodha kitatumika kwa nchi gani. Waziri wake wa Biashara Howard Lutnick anaahidi mapendekezo ifikapo Aprili 1. Ambayo hutoa wakati na nafasi kwa mazungumzo mazuri.