“Mapinduzi ya Kiislamu yaliathiri mapambano ya Afrika Kusini dhidi ya apartheid”

Mwanahabari mkongwe mjini Cape Town, Farid Sayed amesema Mapinduzi ya Kiislamu na kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kulikuwa na athari kubwa kwa mapambano ya Afrika Kusini dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa apartheid.