Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yamebadilisha utaratibu wa dunia: Mhadhiri mwandamizi wa Ghana

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Ghana Dk Munir Mustapha amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamebadilisha mfumo wa dunia na ameyataja kuwa ndiyo yenye nguvu kubwa na ambayo yamekuwa na taathira kubwa imeyozidisha ushawishi wa Iran katika eneo la Magharibi mwa Asia kwa ujumbe wake wa demokrasia ya kidini.