
Huku likihusishwa na uvamizi wa wanamgambo wanaoiunga mkono serikali, shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa Jumatano 5 kuamkia Alhamisi Machi 6, lilifanyika katika kijiji cha Tambi, karibu kilomita mia moja kaskazini mwa Goma, mkoani Kivu Kaskazini, katika eneo linalokaliwa na M23.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani, shambulio kwenye kijiji cha Tambi, mashariki mwa DRC, lililoendeshwa na wanamgambo wa Nyatura Abazungu – Wazalendo wanaopigana pamoja na jeshi la Kongo – lilitokea karibu 4 usiku Jumatano, Machi 6.
Ingawa chanzo cha afya kimetaja idadi ya vifo vya raia 43, idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi, chanzo cha Umoja wa Mataifa kimeiambia RFI, kutokana na kuwa baadhi ya wahanga walifungiwa ndani ya nyumba ambayo ilichomwa moto. Asubuhi ya Alhamisi, Machi 6, “tulienda kwenye eneo la tukio na kuona miili iliyoungua. “Ilikuwa vigumu kuwatambua,” amesema mmoja aliyenusurika katika shambulio hilo, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina.
Watu waliotoroka makazi yao walirejea katika eneo hilo hivi majuzi
Wengi wa waathiriwa – wanaume, wanawake na watoto – ni watu waliokimbia makazi yao ambao walikuwa wamerejea hivi karibuni katika eneo hili linalokaliwa na M23. Wanamgambo wa Wazalendo waliowashambulia wanadaiwa kuwashutumu kwa kushirikiana na wapiganaji hao. Vyanzo kadhaa vya habari vya ndani vinadai kwamba wanamgambo hao wa wazalendo walirejea kwenye ngome zao katika miji ya Bulindi na Butenderi, iliyoko umbali wa kilomita kumi.
Shambulio hilo lilitokea wakati SADC na EAC zimetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika eneo hilo. Kwa siku mbili, mapigano makali yameripotiwa karibu na Masisi kati ya AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na wanamgambo wa Wazalendo.