Manzungumzo kati ya DRC na AFC-M23: Wasaidizi wa Tshisekedi wana mashaka

Mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ulikuwa tena kiini cha majadiliano kati ya Félix Tshisekedi na mwenzake wa Angola João Lourenço siku ya Jumanne, Machi 11, huko Luanda. Angola, ambayo ni mpatanishi katika mgogoro huu, imetangaza nia yake ya kufungua mazungumzo kati ya Kinshasa na kundi la waasi la AFC-M23. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ofisi ya rais wa Angola, mawasiliano yataanzishwa na AFC-M23 ili kuandaa mazungumzo ya moja kwa moja na Kinshasa katika siku zijazo. Lakini tangazo hili linazua maswali. Kwa sasa, DRC imeridhika na “kupokea pendekezo hilo” na inasubiri kuona maelezo kamili, hasa kwa vile bado kuna mambo ambayo hayaeleweki katika tangazo la Angola.

Mkutano wa ngazi ya juu kati ya mamlaka ya Kongo na Angola ulipangwa kufanyika Jumatatu, Machi 10, mjini Luanda, lakini hatimaye haukufanyika. Siku ya Jumanne, Machi 11, mambo yalikwenda haraka. Akiwa na timu ndogo sana iliyomzunguka, rais wa DRC, Félix Tshisekedi, alijikuta katika mji mkuu wa Angola.

Lakini wakati suala la AFC-M23 lilizungumzwa wakati wa mkutano huo, Kinshasa haijabadilisha msimamo wake rasmi: hakuna majadiliano ya moja kwa moja na AFC-M23, kundi linaloungwa mkono na Rwanda, wanasema wasaidizi wa Félix Tshisekedi. Vyanzo kadhaa vya Kongo vinafikia hata kusema kuwa vishangazwa na maudhui ya tamko la Angola, ambalo linataja kufunguliwa kwa mazungumzo ya moja kwa moja na kundi lenye silaha. Kwa upande wa Kongo, wanazungumza tangazo la upande mmoja ambalo halikuratibiwa na Kinshasa.

Chanzo kimoja kimesema: “Mhusika mkuu ni Kigali. Tangazo hii linazua maswali mengi kuliko majibu. Inaonekana kama hii ni ya kufupisha mipango mingine inayoendelea. “Hasa kwa vile, kwa sasa, mpango huu hauna uwazi. Hakuna maelezo au ratiba sahihi. AFC-M23 (Congo River Alliance-March 23 Movement), ambayo pia inawasiliana na Luanda, inakaa kimya na haitoi maoni yoyote.

Mjini Kinshasa, umakini sasa umeelekezwa kwenye mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika leo Alhamisi, Machi 13, pamoja na mkutano kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambao unaweza kufanyika wiki ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *