Man United, Chelsea zapewa wapinzani wabishi Ulaya

Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), limepanga droo ya michuano ya Europa pamoja na Conference League huku Man United na Chelsea zikipewa wapinzani wagumu.

Katika droo hiyo iliyofanyika Nyon, Uswisi muda mfupi baada ya ile ya Ligi Mabingwa Ulaya imeshuhudiwa Manchester United ikipangwa na Real Sociedad katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Europa League, ikiwa ni moja ya timu ngumu kwenye michuano.

United ilifuzu katika hatua ya 16 bora baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ya Europa ambapo ilikusanya jumla ya pointi 18 katika mechi nane ilizocheza ikiwa nyuma pointi moja na Lazio ambao walimaliza vinara wa Ligi hiyo.

Real Sociedad ilifuzu katika hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Midtjylland katika hatua ya mtoano.

Mshindi kati ya Man United au Real Sociedad atakutana na mshindi kati ya Steaua Bucharest au Olympique Lyonnais.

Timu nyingine zitakazokutana katika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Europa

Viktoria Plzen v Lazio

Bodo/Glimt v Olympiacos

Ajax Amsterdam v Eintracht Frankfurt

AZ Alkmaar v Tottenham Hotspur

AS Roma v Athletic Bilbao

Fenerbahce v Rangers

Steaua Bucharest v Olympique Lyonnais

Real Sociedad v Manchester United

Zinazoweza kukutana robo fainali

Bodo/Olympiacos v Plzen/Lazio

AZ/Spurs v Ajax/Frankfurt

Fenerbahce/Rangers v Roma/Bilbao

Bucharest/Lyon v Sociedad/United

Katika michuano ya Conference League Chelsea wenyewe watakutana na Copenhagen katika hatua ya 16 bora huku mshindi kati yao anaweza kukutana na mshindi baina ya Molde au Legia Warsawa.

Chelsea ambayo inapewa nafasi kubwa ya kufika fainali kwenye michuano hii ilimaliza nafasi ya kwanza katika ligi hiyo ikiwa na jumla ya pointi 21 huku ikishinda mechi zote sita bila kupoteza lakini haiwezi kuwa na kazi rahisi dhidi ya wapinzani hao.

Timu nyingine zitakazokutana Conference League

Jagiellonia vs Cercle Brugge

Molde vs Legia Warsaw

Celje vs Lugano

Pafos vs Djurgarden

Panathinaikos vs Fiorentina

Borac vs SK Rapid

Real Betis vs Vitoria SC

Copenhagen vs Chelsea

Zinazoweza kukutana robo fainali

Real Betis or Vitoria SC vs Jagiellonia or Cercle Brugge

Celje or Lugano vs Panathinaikos or Fiorentina

Copenhagen or Chelsea vs Molde or Legia Warsaw

Pafos or Djurgarden vs Borac or SK Rapid.