
Manchester, England. Manchester City inaikaribisha Real Madrid katika Uwanja wa Etihad leo usiku ikiwa ni mechi ya kwanza baina ya timu hizo kusaka tiketi ya kuingia hatua ya 16 bora.
Timu zote mbili zilishindwa kufuzu moja kwa moja katika hatua hiyo na sasa zimelazimika kucheza hatua ya mchujo ili kusaka timu nane za kuungana na nyingine nane ambazo zilishafuzu hatua ya 16 bora.
Historia inaonyesha Man City imekuwa na ubabe dhidi ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na hilo linathibitishwa na mechi 12 zilizopita baina yao kwenye mashindano hayo.
Katika idadi hiyo ya mechi, Manchester City imepata ushindi mara nne, Real Madrid imepata ushindi mara tatu na zimetoka sare mara moja.
Wakati Manchester City ikiwa imefunga mabao 21 katika mechi hizo 12 ambazo timu hizo zimewahi kukutana, Real Madrid imefunga mabao 18.
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ni msimu uliopita katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo mechi zao mbili zilimalizika kwa sare ya mabao 3-3 lakini Real Madrid ikapata ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 na kusonga mbele.
Mchezo wa leo utachezeshwa na refa Clement Turpin kutoka Ufaransa.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni Sporting CP itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Borussia Dortmund, Juventus watacheza na PSV Eindhoven kwenye uwanja wa Allianz, Turin, Italia.
Mechi zote za hatua ya mtoano:
Real Madridvs Manchester City
Dortmund vs Sporting Lisbon
Atalanta BC vs Club Brugge
AC Milan vs Feyenoord
SL Benfica vs AS Monaco
PSV Eindhoven vs Juventus FC
Bayern Munich vs Celtic FC
Paris Saint Germain vs Stade Brest