
Misri siku ya Jumapili imefutilia mbali majaribio ya kuanzisha serikali pinzani nchini Sudan, ikionya kwamba hatua kama hizo zinadhoofisha “umoja, mamlaka na uadilifu wa eneo” la nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Sudani imekuwa katika vita kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwa karibu miaka miwili, na kuitumbukiza nchi hiyo katika kile ambacho Umoja wa Mataifa unakielezea kuwa moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu katika kumbukumbu za hivi karibuni.
Wiki moja iliyopita, RSF na washirika wake walitia saini mkataba nchini Kenya unaotangaza kuundwa kwa “serikali ya amani na umoja” katika maeneo wanayodhibiti.
“Misri inaeleza kukataa kwake jaribio lolote linalotishia umoja, mamlaka na uadilifu wa eneo la Sudani ndugu, ikiwa ni pamoja na harakati za kuunda serikali pinzani ya Sudan,” Wizara ya Mambo ya Nje yenye makao yake makuu mjini Cairo imesema katika taarifa yake Jumapili.
Imeongeza kuwa vitendo kama hivyo “vinafanya hali kuwa ngumu nchini Sudani, vinatatiza juhudi zinazoendelea za kuunganisha maono ya kisiasa na kuzidisha mzozo wa kibinadamu.”
Misri pia imetoa wito kwa “wadau wotenchini Sudani kutanguliza maslahi ya juu ya kitaifa ya nchi na kushiriki vyema katika kuanzisha mchakato wa kina wa kisiasa (amani) bila kutengwa au kuingiliwa na mataifa ya kigeni.”
Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty alitoa msimamo huo huo katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Sudani Ali Youssef.
Mstari mwekundu
“Uadilifu wa eneo la Sudani ni mstari mwekundu kwa Misri,” alisema, akiongeza kuwa nchi yake “inakataa wito wowote wa kuanzisha miundo mbadala nje ya mfumo wa sasa.”
Hatua ya wanamgambo hao kuunda serikali pinzani imekosolewa vikali, ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambaye alionya kwamba “itaongeza zaidi mgawanyiko wa Sudani”.
Saudi Arabia, ambayo tayari imeshapatanisha mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya pande zinazozozana, pia imekataa hatua hiyo ya RSF.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa na Shirika la Habari la serikali ya Saudi Arabia, Wizara ya Mambo ya Nje ya Riyadh ilionya dhidi ya “hatua zozote zisizo halali au hatua zinazochukuliwa nje ya mfumo wa taasisi rasmi.”
Kuwait iliunga mkono msimamo huo siku ya Ijumaa, ikisema kuwa inakataa “hatua zozote zisizo halali zilizochukuliwa nje ya mfumo wa taasisi halali za serikali” nchini Sudani, na kuzitaja kuwa “tishio kwa umoja wake wa eneo.”
Katika mazungumzo ya Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa, Qatar, jirani wa Ghuba ya Saudi Arabia, pia ilielezea kuunga mkono “umoja na uadilifu wa eneo la Sudani.”
Falme za Kiarabu, zinazoshutumiwa mara kwa mara kwa kusambaza silaha kwa RSF – tuhuma ambazo imekanusha – bado hazijatoa maoni yoyote.