Mamilioni ya watu wameendelea kutoroka makazi yao nchini DRC: OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya  Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kuwa mamilioni ya watu wanaendelea kuyahama makazi yao Kivu Kaskazini na Kivu Kusini nchini DRC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Huko  Kivu Kaskazini inaripotiwa kuwa  watu 110,000 wameondoka katika kambi za wakimbizi huko Goma na kuanza kuhamia katika vijiji vya Masisi, Rutshuru na Nyiragongo.

OCHA na washirika wake wa kibinadamu pia wana wasiwasi kuhusu uporaji unaoendelea wa miundombinu katika kambi za wakimbizi wa ndani.

Hali hii inasababisha kuporwa kwa vifaa vya kibinadamu katika maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa maji, vituo vya afya, na vituo vya matibabu ya kipindupindu, na kusababisha hasara kubwa ya kifedha na kupunguza uwezo wa kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliopoteza makazi yao.

Soma piaMamilioni ya watu wanaendelea kuyahama makazi yao mashariki ya DRC.

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kibinadamu bado wana wasiwasi na makataa ya saa 72 yaliyotolewa na wawakilishi wa M23 tarehe 9 Februari kwa watu waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi  huko Goma kuondoka na kurejea vijijini mwao.

Mnamo Jumatatu (10 Feb), M23 ilitoa taarifa ikieleza kwamba inaunga mkono kikamilifu na inahimiza raia kurejea kwa hiari lakini hailazimishi mtu yeyote kurudi bila yeye kuwa na hakikisho la usalama wake.

Umoja wa Mataifa unasema  lazima watu warejee katika makazi yao kwa hiari.