Mambo saba yaliyobamba harusi ya Aziz Ki na Hamisa Mobetto

Dar es Salaam. Ilikuwa bab’kubwa. Ndivyo ilivyokuwa katika sherehe ya kupongezwa kwa maharusi, Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI na mwanamitindo, Hamisa Mobetto iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.

Wawili hao waliooana Jumapili iliyopita Mbweni, ikiwa ni siku moja tangu kufanyika kwa tukio la utolewaji wa mahari, walipongezwa katika sherehe kubwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Super Dom Masaki na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali.

                       

Miongoni mwa mastaa waliohudhuria sherehe hiyo iliyopambwa na burudani ya muziki wa Bongofleva na taarabu ni pamoja na wachezaji wa soka, wanamitindo, wabunifu wa mavazi na watu wengine mashuhuri ambapo licha ya kuwa na idadi ya watu wanaoweza kuhesabika kwa urahhisi, lakini sherehe ilifana na Mwanaspoti inakuletea baadhi ya yaliyojiri ukumbini.

Waliohudhuria 

Baadhi ya wasanii waliohudhuria ni pamoja na Marioo na mchumba wake Paula, Lulu Diva, Wema Sepetu, Jackline Wolper, Masha Love, Gigy Money, Nandy, Christian Bella, Gabo ze Gamba, Mzee Yusuf na mkewe Leila Rashid, Husna Sajenti, wabunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka na Martin Kadinda, 

                   

Baadhi ya wachezaji wa Yanga akiwamo kinara wa mabao, Clement Mzize, viongozi wa kklabu huiyio wakiongozwa na Rais Injinia Hersi Said, Ali Kamwe, Meneja wa Kitengo cha ‘Digital’ wa klabu hiyo, Priva Abiudi ‘Privaldinho’  pamoja na Haji Manara na mke wake Zaylissa nao walishuhuria pati hiyo, huku wakijaribu kumfurahisha bibi harusi pamoja na mumewe kwa staili tofauti tofauti.

Nguo mara mbili

Licha ya kuingia ukumbini kwa kuchelewa, kwani waliingia saa 6 usiku na kumlazimisha MC Gara B kupelekea ratiba haraka haraka ili iendane na muda kutokana na ukweli waalikwa walikaa na kuchoka kuwasubiri wahusika hao wenye shughuli yake.
Muda wakuingia maharusi, kila mmoja kwa wakati wake, alianza kuingia Aziz Ki kisha baadaye akafuata Hamisa Mobetto. 

                    

Rangi ya nguo waliyokuwa wamevalia ni nyeupe hii ilikuwa raundi ya kwanza kisha baadaye wakaenda kubadilisha na kuvaa nguo za rangi ya blue bahari, kitendo hiki kiliwavutia wageni waalikwa waliwapigia makofi na vigelegele kwa wingi.

Wakosa viti 

Kutokana na viti livyokuwa vimepangwa kwenye ukumbi, vilikuwa vimeenea vyote kwa kukaliwa kwa watu, lakini kuna watu wengi walikosa viti vya kukaa, hii huenda ikawa wapangaji wa viti walipanga viti bila kupata idadi ya wageni waalikwa. 
Kitendo hiki kiliboa baadhi ya wageni walioalikwa hasa wale waliokuwa wamesimama mwanzo wa sherehe hadi mwisho.

                     

Ukumbi kawaida sana 

Ni hali ya tofauti ambayo wageni wengi waalikwa wamekutana nayo, walitegemea wakiingia ukumbini watakutana na ukumbi uliopambwa vizuri na ukavutia zaidi, lakini hii haikuwa hivyo kwani ukumbi umepambwa kawaida sana na wametumua rangi moja ya pink mpauko na kusababisha kuwa na giza kidogo. Na maua yaliyowekwa mezani yalikuwa mengi kuliko vinywaji.

Wakosa chakula

Wakati Mc Gara B akiwa anaendelea na ratiba ya sherehe, wapo wageni waalikwa wakiwamo wachezaji wa Yanga waliinuka kwenda nje kutafuta chakula kutokana na kuchelewa kuruhusu watu kula licha ya kuwa saa 8 usiku.

Ikawa sasa wageni waalikwa wanajiinua wenyewe kwenda kula kabla ya MC kufikia kipengele hicho, muda  wa chakula ulipofika saa 9 usiku  chakula kilikuwa kimeisha na baadhi ya wageni waalikwa walikosa chakula.

Yanga wageni wafunika wazawa 

Wachezaji wa Yanga wa kigeni wakiongozwa na Khalid Aucho, Kennedy Musonda, Yao Kouassi, walichangamka tofauti na wazawa kama Mzize, Kibwana Shomary, Denis Nkane, Bakari Mwamnyeto na hata hivyo wale wa kigeni walikuwa wamepigilia suti nyeusi huku wa Kibongo walivaa suti rangi ya kijani kibichi.

Vijembe ukumbini 

Ilikuwa ni mwendo wa vijembe nyimbo za  vijembe ukumbini, pale zilipoingwa nyimbo hizo za taarabu, wageni waalikwa wanawake baadhi waliinuka kwenye viti vyao na kucheza, ndipo Zaylissa mke wa Manara alienda kumtunza Leila Rashid mke wa Mzee Yusuf, kumtunza huko alikuwa anazitupia  walipokuwa wanacheza waliowahi kuwa wake wa Manara Rushayna na Rubyna.

Nao ndipo walipojibu mapigo ya kucheza kwa kushikana huku wakimsogelea muimbaji na kumtunza.

Kurushana roho huko hawakuishia hao tu, bali Giggy Money na Masha Love nao walikuwa wanatambiana kwa kucheza.
Licha ya dosari chache zilizojitokeza, lakini sherehe ya Aziz Ki na Hamisa Mobetto ilikuwa bab’kubwa.