Mali yaanzisha jitihada mpya ili kuweza kuachiliwa kwa raia waliotekwa tangu mwezi Aprili 2024

Tangu Jumapili, jitihada mpya za ndani zimekuwa zikiendelea ili kuhakikisha kuachiliwa kwa dazeni kadhaa za raia wanaoshikiliwa mateka tangu mwezi Aprili 2024.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu katika kikanda, Serge Daniel

Jitihada mpya za kuhakikisha kuachiliwa kwa makumi ya watu wanaoshikiliwa mateka tangu mwezi Aprili 2024 katika eneo la Mopti zinaongozwa na afisa mkuu katika utawala wa Mali, ambaye ofisi yake iko katika eneo la Bandiagara.

Angalau machifu wawili wa vijiji kutoka mkoa huo wanahusika katika mazungumzo. “Tunapozungumza kidogo, ndivyo mazungumzo yanavyopiga hatua zaidi,” kinabainnisha chanzo kilicho karibu na suala hilo.

Wanajihadi wanadhibiti vijiji kadhaa katika eneo hili. Watu wa kiasili wanaoishi huko hutii sheria zao. Haijafutiliwa mbli kwamba kifungu hiki kinaweza kujumuishwa katika makubaliano yanayowezekana ya kuachiliwa kwa mateka.

Miongoni mwa kundi la raia waliotekwa nyara, baadhi yao wanashutumiwa kwa kulifahamisha jeshi ngome za wanajihadi. Katika suala hili, wajumbe katika mazungumzo hayo wanapaswa pia kuwahakikishia wahusika wa utekaji nyara hu kuhusiana na usalama wao na kutofunguliwa mashitaka mbele ya mahakama.

Raia hao walitekwa nyara mwezi Aprili 2024. Walikuwa ndani ya mabasi matatu yaliyokuwa yakisafiri katika eneo la kati la Mali. Hapo awali, watu wenye silaha, wanaoshukiwa kuwa wanajihadi, walisimamisha mabasi. Baadhi ya abiria waliachiwa, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kisha msafara huo ukaelekea kwenye msitu uliopo kati ya miji ya Bandiagara na Bankass.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *