Mali: Watu kumi na watano waluawa na jeshi na Wagner katika eneo la Timbuktu

Nchini Mali, takriban watu kumi na watano wameuawa kikatili na jeshi la Mali na wasaidizi wake wa kundi la Wagner kutoka Urusi. Ukatili dhidi ya wanawake pia unaripotiwa. Mauaji hayo yalitokea kati ya siku ya Jumatatu 10 na Jumatano 12 Februari, katika wilaya ya Goundam, mkoani Timbuktu. Eneo ambalo wanajihadi kutoka Kundi linalodai Kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM), wanaohusishwa na al Qaeda, wapo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Doria ya Kikosi cha Wanajeshi wa Mali (FAMA) na Wagner iliondoka Goundam siku ya Jumatatu Februari 10 asubuhi, siku ya maonyesho. Tangu wakati huo ilipitia kambi za watu wanaohamahama na vijiji kadhaa: Tabagout, Erabedje, Razelma, kisha Zouera na Gouber siku ya Jumanne, na Tinadanda siku ya Jumatano.

Vyanzo vingi vya ndani vilivyowasiliana na RFI vinaripoti angalau mauaji ya kutisha watu kumi na tano. “Si miili yote iliyopatikana,” moja ya vyanzo hivi inaelezea, wakati watu kadhaa walichukuliwa na kupelekwa na wanajeshi FAMA na wasaidizi wao Wagner. Operesheni ya kijeshi bado inaendelea.

Wanawake pia walifungwa kamba na kufanyiwa dhulma zisizoelezeka. Kesi za ubakaji huko Tabagout zimeripotiwa na vyanzo kadhaa, lakini hazihusishi wanajeshi wote: ni ngumu kujua ikiwa taarifa hizi ni za kupotosha kwa baadhi ya watu, kwa kulaumu jeshi na Wagner, au kinyume chake kupunguza uhalifu unaofanywa napande hizo mbili kwa upande wa wengine, unyanyasaji wa kijinsia kwa kiasi kikubwa ni mwiko, haswa katika maeneo ya kijadi.

Hapo awali, kesi za ubakaji zilizotekelezwa na mamluki wa Wagner tayari zimerekodiwa, haswa huko Nia-Ouro na Moura mnamo mwaka 2022, ambapo ubakaji huu ulikuwa mkubwa.

Ushuhuda pia unaripoti kambi kuporwa na kuchomwa moto, na picha zinazounga mkono hili, pamoja na magari kuibiwa au kuharibiwa na watu waliotishwa na hofu wakikimbia. Kwa hali yoyote, vyanzo vinaripoti tu mauaji ya kikatili, bila mapigano. lilipoulizwa na RFI kuhusu kesi hizi, jeshi la Mali halikujibu.

Eneo la Goundam linajulikana sana na wanajihadi wa JNIM, wanaohusishwa na al-Qaeda.