
Wapiganaji wawili kutoka Movement for the Salvation of Azawad (MSA, wanaounga mkono utawala wa kijeshi) wameuawa siku ya Jumamosi, Machi 22, 2025, kwa kilipuzi kilichotegwa barabarani katika eneo la kaskazini. Makundi ya wanajihadi yanashutumiwa kwa kutega bomu la ardhini, ambapo mlipuko wake pia umejeruhi wapiganaji wa MSA.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel
Kulingana na Vuguvugu la MSA, tukio hilo lilitokea kati ya miji ya Ansongo na Menaka kaskazini mwa Mali. Wapiganaji wawili waliouawa ni kutoka vuguvugu lenye silaha ambalo linaunga mkono utawala wa kijeshi wa Bamako. Walikuwa wakikitoa ulinzi, pamoja na jeshi la Mali, msafara magari yaliyokuwa yakisheheni chakula.
Kwa mujibu wa habari zetu, mabomu yaliyotegwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi pia yaliwajeruhi wanajeshi waliokuwa wakitoauminzi wa msafara wa magari yaliyokuwa yakibebea chakula. Katika jimbo la Menaka, kundi kuu la wanajihadi lililopo ni kundi la Islamic State. Linadhibiti maeneo kadhaa, linaajiri wapiganaji miongoni mwa wakazi wa eneo hilo na hadi sasa limejaribu bila mafanikio kudhibiti eneo la Menaka.
Wanaopingana nao ni jeshi la Mali, Wagner, kundi la wanamgambo wa Urusi, na MSA, linaloundwa na wakazi wa jimbo hilo. Wakati kundi la MSA likiunga mkono operesheni za wanajeshi wa serikali, haswa kaskazini-mashariki mwa Mali, kundi kubwa lenye silaha, Azawad Liberation Front (FLA) linadai kuwa linaunga mkono uhuru na linapigana na jeshi la Mali.