
Nchini Mali, mpango wa DDR-1 wa “kupokonya silaha wapiganaji, kuwarejesha katika maisha ya kiraia, kuwaunganisha katika vikosi vya ulinzi na usalama” ulizinduliwa rasmi siku ya Jumanne, Februari 11, na serikali ya mpito ya Mali.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Mpango huo unatoa nafasi kwa wapiganaji kutoka makundi yenye silaha, hasa kutoka kaskazini mwa Mali, lakini pia kutoka katikati kuingizwa katika katika jeshi la nchi. Mchakato huu wa DDR ambao ulianza mwaka wa 2015 kama sehemu ya makubaliano ya amani, haujawahi kukamilika. Makubaliano ya amani tangu wakati huo yamevunjwa na utawala wa kijeshi uliopo, ni makundi tu yanayojiita “republican”, yakiwa yamechagua kushirikiana na mamlaka ya mpito ya Mali, yataweza kunufaika na mpango huo.
Walengwa wakuu ni wapigaaji wa Gatia (Touareg Imghad na Allied Self-Defense Group) wa Jenerali El Hadj Ag Gamou, gavana wa sasa wa Kidal, na wale wa MSA (Movement for the Salvation of Azawad) ya Moussa Ag Acharatoumane, waliopo hasa katika maeneo ya Ménaka na Gao. Makundi haya mawili tayari yanapigana pamoja na jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Wagner kutoka Urusi.
Makundi mengine yenye silaha yasiyo muhimu sana pia yanahusika: “MAA CPA”, “CMFPR1, 2 na 3”, wawindaji wa jadi wa Dozo wa kundi la Dan Na Ambassagou, pamoja na wapiganaji kutoka makundi ya kujilinda ya Fulani.
Askari 2,000 wa daraja la pili
Hakuna takwimu za kina kwa makundi haya, lakini kwa jumla, Wizara ya Maridhiano ya Kitaifa ya Mali inaonyesha kuwa wapiganaji 2,000 watajumuishwa katika jeshi “kama askari wa daraja la pili.” Wengine elfu kadhaa watanufaika na mpango wa kurejeshwa katika maisha ya kiraia.
Vitengo hivi vilipangwa awali kwa mwaka wa 2024. Hakuna maelezo yoyote ambayo yamewasilishwa kwenye ratiba mpya iliyopangwa, lakini lengo ni “kwenda haraka”, anaeleza Moussa Ag Acharatoumane wa MSA, ambaye “amekuwa akingojea hili kwa muda mrefu”. Mchakato wa DDR una faida katika suala la mshahara, kutambuliwa, “hadhi juu ya yote”, anasisitiza kiongozi huyo wa kisiasa na kijeshi, pia mjumbe wa Tume ya Ulinzi ya Baraza la Kitaifa la Mpito (NTC), ambaye anabainisha kuwa baadhi ya wapiganaji wake tayari waliunganishwa na jeshi katika miaka ya hivi karibuni.
“Upatanisho endelevu”, lakini FLA haihusiki
Mchakato huu “hauishii tu kwa ujumuishaji wa wapiganaji wa zamani katika vikosi vya ulinzi,” ametangaza Waziri wa Maridhiano ya Kitaifa, Jenerali Ismaël Wagué. Pia unahusu kujenga hali ya kuaminiana kati ya wahusika na kuendeleza upatanisho wa dhati na wa kudumu. “
Makubaliano ya amani ya 2015 yakiwa yamevunjwa na utawala wa kijeshi uliopo, makundi yenye silaha yaliyotia saini, leo yamekusanyika ndani ya FLA (Azawad Liberation Front), bila shaka hayana wasiwasi. Sasa wanachukuliwa kuwa “magaidi” na mamlaka ya mpito ya Mali, wamechukua silaha tena kwa madai yao ya uhuru.