Mali: Wagner yafungasha virago na nafasi yake kuchukuliwa na Africorps

Kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner linafungasha virago vyake kutoka Mali na mamluki wake baada ya miaka mitatu na nusu ya uwepo wake nchini humo. Nafasi yake inachukuliwa na Africa Corps, kundi lingine la wanamgambo wa Kirusi ambalo liko chini ya mamlaka ya Kremlin.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu kutoka Bamako, Serge Daniel

Huko Bamako, kulingana na duru rasmi, hakuna chanzo chochote tulichowasiliana nacho kinachothibitisha au kukataa kuondoka kwa mamluki wa Urusi wa kundi la Wagner nchini Mali. Kama tunavyojua, utawala wa kijeshi wa Mali daima umekuwa ukikataa uwepo wa mamluki hawa nchini Mali, ukipendelea kutumia neno “wakufunzi wa Kirusi.”

Kuhusu Wagner, kuondoka kwa wanajeshi hao kutoka Mali kumetangazwa baada ya wao kuwepo nchini humo zaidi ya miaka mitatu. Nafasi yao itachukuliwa na kundi lingine la wanamgambo wa Kirui: Africa Corps. Hili pia ni kundi la wanamgambo wa Kirusi linalotetea maslahi ya nje ya Urusi barani Afrika. Africa Corps ambayo ina wafanyikazi wa zamani wa Wagner na haswa waajiri wapya, iko chini ya mamlaka ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Haya ni mabadiliko kidogo mtu anapokumbuka kwamba Wagner ilikuwa ikiongozwa kwa uthabiti na Yevgeny Prigozhin, ambaye kwa hakika alikuwa karibu na Kremlin lakini mwenye nia kali, kabla ya kifo chake katika ajali ya ndege mnamo mwezi wa Julai 2023.

Kwa kuondoka Mali, Wagner imetoa ripoti nzuri ya uwepo wake nchini Mali. Jambo lingine la mzozo ni kwamba kama uwepo wa Wagner ulisaidia kuutwaa tena mji wa Kidal kutoka mikononi mwa waasi wa Mali, usalama haujarejeshwa katika sehemu kubwa ya Mali. Zaidi ya hayo, Wagner imeshutumiwa kwa dhuluma dhidi ya raia na mashirika kadhaa ya haki za binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *