Mali: Vyama vya kisiasa vinaitisha kuandamana tena Mei 9 dhidi ya serikali ya mpito

Nchini Mali, vyama vya kisiasa vinaitisha kufanya maandamano mapya Mei 9. Mnamo Mei 3, mandamano yao yalizuiwa na watu waliohamasishwa na mamlaka ya mpito na kuingilia kati kwa polisi. Hii ilizua matukio ya maandamano yasiyokuwa ya kawaida mbele ya Palais de la Culture huko Bamako.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa vyama ambao walikutana siku ya Jumatatu, waliamua kuendeleza shinikizo, kupinga kufutwa kwao, lakini pia kutaka kumalizika kwa kipindi cha mpito na kurudi kwa utaratibu wa kikatiba. Maandamano mapya yametangazwa siku ya IjumaaMei 9, saa 8 mchana, mbele ya Mnara wa Uhuru.

Wakati huu, maandamano hayatafanyika katika chumba lakini katikati ya barabara, katikati ya mji mkuu wa Mali, kwenye eneo la kiishara la mapambano yaliyoendeshwa na raiawa Mali dhidi ya ais wa zamani Ibrahim Boubacar Keïta (2013-2020) au dhidi ya vikwazo vya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, kwa mfano.

“Tunachukua hatua ili kuonyesha uwezo wetu wa uhamasishaji,” anaelezea kiongozi wa chama kilichojihusisha sana, akiongeza kuwa mawasiliano yamefanywa na wadau wengine – wa kidini, wa jadi au wa kiraia – kujaribu kushirika maandamano hayo. “Watu wana hatima yao mikononi mwao!” “,  anasema waziri wa zamani.

Changamoto hii kwa wanajeshi walioko madarakani ni “changamoto kwetu pia,” amesema kiongozi wa chama kikuu cha siasa, mwenye kujiamini lakini mwenye shauku ya kuhifadhi “umoja wa vyama” na kufanikiwa “kuwaunganisha wananchi wenzetu nyuma ya mapambano yetu “.

“Mtego wa vurugu”

Hata hivyo, kila mtu anatarajia maandamano yaliyotangazwa kupigwa marufuku na mamlaka ya mpito. “Wana wasiwasi, hofu imetanda pande zote,” anasema waziri huyo wa zamani, ambaye anaongeza kuwa “mipango B na C” tayari iko tayari. Katika tukio la kupiga marufuku, “tutaendelea kufuata kisheria,” kiongozi mwingine wa chama pia anahakikisha: maandamano hayo yatafutwa na waandaaji wake, kama maandamano ya Jumamosi iliyopita. “Hatutaki kuingia kwenye mtego wao, hatutafanya vurugu.”

Siku ya Jumamosi na Jumapili ya wiki iliyopita, matukio mawili yaliyoandaliwa na waandamanaji katika Palais de la Culture na Jumba la wanahabari yalizuiwa. Tukio la kwanza lilisambaratishwa, tukio la pili, na watu binafsi waliohamasishwa na mamlaka (ikiwa ni pamoja na mjumbe wa Baraza la Taifa la Mpito na maofisa misheni kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maridhiano). Waandishi wa habari walikuwa hata “walishambuliwa kimwili na kwa maneno,” kulingana na taarifa ya hasira kutoka Jumba la wanahabari. Vyama vya siasa vinakusudia kuomba kuachishwa kazi kiutawala kwa maafisa hao na kuwachukulia hatua za kisheria.

Vitisho

Vurugu kutoka kwa wafuasi wa utawala wa kijeshi na uwezekano wa kupigwa marufuku kwa maandamano yaliyopangwa kufanyika Ijumaa sio vitisho pekee vinavyowakabili wanaharakati wanaounga mkono demokrasia. Vyanzo vingi vinahofia kwamba mamlaka ya mpito itachukua hatua haraka kupunguza uhuru wa kukusanyika na kuandamana, au hata kusimamisha shughuli za kisiasa nchini, kama ilivyofanya kwa miezi mitatu mwaka jana.

Katika hatua hii, hakuna tangazo ambalo limetolewa katika suala hili. “Tutakuwa tukifuatilia habari za ORTM na taarifa za vikao vya Baraza la Mawaziri la Jumatano,” chanzo kingine kutoka vuguvugu la maandamano kimesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *