Mali: Upinzani waapa kukabiliana na jeshi dhidi ya nia yake ya kusalia madarakani

Mswada, uliopitishwa siku ya Jumatano, Juni 11, na Baraza la Mawaziri, unatoa nafasi ya kumpa Jenerali Assimi Goïta “muhula wa miaka mitano, unaoweza kufanywa upya kuanzia mwaka 2025.” Hali ya usalama nchini Mali na Sahel inatajwa kuhalalisha uamuzi huo wa muswada huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kusalia huku madarakani kwa rais na taasisi zote za mpito, bila uchaguzi na bila kikomo cha muhula, ulipendekezwa mwishoni mwa mwezi Aprili kufuatia “mashauriano kati ya wadau nchini,” yaliyoratibiwa na mamlaka. Viongozi wa vyama vya siasa wanaonyesha hasira zao.

“Tunasitasita kati ya hasira na kutojali,” waziri wa zamani amesema, “kwa sababu hii ilionekana mapema na hatutarajii chochote kutoka kwa mamlaka.” Wakati wanajeshi walio madarakani nchini Mali waliahidi kuilinda na kuifanyia mageuzi nchi hiyo kabla ya kufanyika uchaguzi haraka, kiongozi wa chama kilichofutwa amebainisha kuwa wanageuka kuwa “wanasiasa wa aina tofauti.” Tukikumbuka “kalenda zote za uchaguzi zilizoanzishwa kiserikali na kukiukwa kiserikali,” chanzo hiki kinahoji: “Ni mwanasiasa gani wa kiraia amesaliti kiasi hiki?”

Kinyume na katiba

Wapinzani kadhaa wanaona hali ya kukiuka katiba ya mswada huo na kuendelea kwa mamlaka bila uchaguzi, lakini hawako chini ya udanganyifu wowote tena. “Nia ya kweli ya jeshi ni kubaki madarakani,” anasema waziri wa zamani aliyekatishwa tamaa, “mengine ni mapambo tupu.”

“Wakati ambapo wanajeshi wetu wanauawa, wanafikiria tu kuhusu furaha ambayo unyakuzi wa mamlaka unawaletea,” anakashifu waziri mwingine wa zamani, ambaye anashutumu “mapinduzi mengine, wakati huu ya kikatiba.” “Mali ina thamani zaidi ya mamlaka iliyoibiwa,” anaongeza kiongozi huyo ambaye ni nguzo ya vuguvugu linalounga mkono demokrasia, “lakini watu, mapema au baadaye, watawanyang’anya kile walichofikiri wanaweza kushikilia kwa nguvu.” 

“Tunaingia katika moja ya awamu ya giza zaidi ya nchi yetu,” hatimaye anabainisha kiongozi mwingine wa upinzani, akitoa wito wa kuendelea kupambana “kwa njia zote zinazowezekana.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *