Mali: Shambulio la wanajihadi laua kumi na sita katika eneo la Ségou

Nchini Mali, watu 16 waliuawa siku ya Jumatano, Februari 12 katika kijiji kilicho katika eneo la Macina, katika jimbo la Ségou, katikati mwa nchi. Shambulio hili bado halijadaiwa na kndi lolote, lakini vyanzo vya ndani kwa kauli moja vinalihusisha na kundi la Katiba Macina ya Jnim, Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu, lenye mafungamanona Al Qaeda. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katiba Macina inaweka sheria yake katika vijiji vingi katika sehemu hii ya eneo la Mali. Maeneo ambayo yanakataa kutii sheria za kundi hili mara kwa mara yanakumbwa na matatizo.

Kijiji cha Berta, katika wilaya ya Saloba, ndicho kililengwa na shambulio hilo.

Kulingana na shuhuda za vyanzo vingi vya ndani – viongozi waliochaguliwa, wakaazi wa eneo hilo, wawakilishi wa jamii mbalimbali – wanajihadi walifanya shambulio lao wakati wa safari ya pamoja ya uvuvi kwenye maji ya nyuma (maji yaliyotuama au yanayosonga polepole, ambayo mara nyingi hupatikana mbali na mkondo).

Watu 16 waliuawa, kadhaa kujeruhiwa. Wanakijiji walichukuliwa na wanajihadi, wengine bado hawajulikani waliko.

Hatimaye, shuhuda zinaripoti uharibifu, ikiwa ni pamoja na mikokoteni iliyochomwa.

Mikataba ya ndani

Jumuiya ya Saloba iko katika eneo la kati ya mto katika eneo la Macina.

Katika miaka ya hivi karibuni, maeneo kadhaa katikati mwa Mali yameacha kusaini mikataba ya ndani na Katiba Macina ya Jnim. Ili kuweza kuzunguka au kulima mashamba yao, wanakijiji wanakubali kufuata sheria za wanajihadi: malipo ya kodi, suruali fupi kwa wanaume na hijabu kwa wanawake, namna ya kusali…

Vijiji vinavyokataa kutii sheria za kundi hili vinalengwa mara kwa mara na wanajihadi. Hii ndio kesi ya wilaya ya Saloba.

Miongoni mwa waathiriwa wa shambulio la Jumatano ni wanakijiji wa kawaida, lakini pia wawindaji wa jadi wa Dozo, ambao wanajukumu kama kundi la kujilinda dhidi ya wanajihadi.

Walipowasiliana na RFI, jeshi la Mali halikujibu.

Zantiguila

Hata hivyo, siku ya Alhamisi asubuhi, Jnim ilidai udhibiti wa ngome mbili za kijeshi huko Zantiguila, katika eneo la Koulikouro. Shambulio lililothibitishwa na vyanzo vya ndani. Jnim haijatoa taarifa zozote kuhusu idadi ya vifo au majeruhi, na jeshi la Mali halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo.