
Nchini Mali, imepita mwaka mmoja, tangu kutiwa saini kwa mkataba kati ya wanasiasa na viongozi wa mashirika ya kiraia, kushinikiza uongozi wa kijeshi, kurejesha uongozi wa kikatiba.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Hii inakuja baada ya wanajeshi kuchukua madaraka Agosti mwaka 2020, na mpango wa kurejeshwa madaraka kwa raia, kuahirishwa mara kadhaa.
Tarehe ya mwisho ya jeshi kurejesha madaraka kwa raia, Machi 26 mwaka 2024, lakini hilo halikufanyika.
Miongoni mwa wanasiasa wanaohusika na shinikizo za kutaka kurejeshwa kwa uongozi wa kikatiba ni Ismaël Sacko, anayeishi nje ya nchi anasema hali imeendelea kuwa mbaya na haifahamiki ni lini jeshi litaondoka madarakani.
Sacko, amelalamikia kuendelea kukamatwa na kuteswa kwa wakosoaji wa ungozi wa kijeshi na uhuru wa vyombo vya Habari kuminywa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Uongozi wa jeshi, umekuwa ukisema, kipaumbele chake kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kuna amani katika nchi hiyo.