Mali: Mashirika ya kiraia yaituhumu serikali kwa kujaribu kuyaminya

Makundi zaidi ya 100 ya mashirika ya kiraia na vyama vya siasa nchini Mali, vimeutuhumu utawala wa kijeshi kwa kujaribu kuwaminya kama ilivyofanyika kwenye mataifa jirani ya Burkina Faso na Niger.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Makundi hayo pia yametaka kuahirishwa kwa majadilinao ya kitaifa yaliyoandaliwa na utawala wa kijeshi ili kupitia mkataba kuhusu vyama vya siasa ulioridhiwa katika kongamano la mwaka 2022.

Taifa hilo la ukanda wa Sehel limekuwa chini ya uongozi wa kijeshi tanguj mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021, na limeshuhudia utovu wa usalama tangu mwaka 2012 kutokana na ongezeko la makundi ya kijihadi.

Onyo la vyama hivi vya siasa limetolewa baada ya utawala wa kijeshi kushindwa kurejesha uongozi wa kiraia kama ulivyoahidi mwezi machi mwaka jana, badala yake ukatangaza kuahirisha ichaguzi wa rais bila kutaja terehe nyingine.

Katika taarifa yao, vyama vya siasa vimesema vinahofia uwanja wa kisiasa kufinywa na wanajeshi na kwamba kuna kila dalili kuwa huenda wakatangaza kuzuia shughuli zozote za kisiasa, wakihoji kwanini utawala unataka majadiliano mengine kuhusu mustakabali wa kisiasa wa taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *