
Rais wa mpito wa Mali, Jenerali Assimi Goïta, ameamua kusitisha “hadi itakapochukliwa hatua nyingine, kwa sababu za usalama wa umma, shughuli za vyama vya kisiasa katika nchi nzima.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Hatua hiyo inatumika kwa shughuli za vyama vya kisiasa na kwa shughuli za shirika lingine lolote linalodai kuwa la kisiasa.
Taarifa hiyo imetangazwa kwa umma katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya serikali ya ORTM kufuatia mkutano wa Baraza la Mawaziri siku ya Jumatano, Mei 7. Amri ya rais itachapishwa katika Jarida Rasmi.
awali vyama vya kisiasa vilitisha kufanya maandamano mapya Mei 9. Mnamo Mei 3, mandamano yao yalizuiwa na watu waliohamasishwa na mamlaka ya mpito na polisi kuingilia kati. Hii ilizua matukio ya maandamano yasiyokuwa ya kawaida mbele ya Palais de la Culture huko Bamako.