Mali: Maandamano ya kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia yafanyika

Maandamano makubwa yamefanyika nchini Mali, kushinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia baada ya uongozi wa kijeshi kuandaa mazungumzo ya kitaifa, yaliyopendekeza Jenerali Assimi Goïta kuendelea kusalia madarakani.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yaliyfanyika Jumapili jijini Bamako, yalipangwa na wanasiasa vijana na viongozi wa mashirika ya kiraia licha ya jaribio la maafisa wa usalama kujaribu kuwazuia kuendelea na mpango wao.

Wanasiasa na wanaharakati hao, wamesisitiza kurejea kwa mfumo wa uongozi wa kidemokrasia na sheria nchini Mali na kumalizika  kwa uongozi wa kijeshi.

Aidha, wamekataa mapendekezo ya mazungumzo yaliyoandaliwa na uongozi wa kijeshi, yaliyopendekeza kuwa Jenerali Assimi Goïta, awe rais wa nchi hiyo kwa muhula wa miaka mitano, bila ya kufanyika kwa uchaguzi.

Pendekezo lingine ambalo limekataliwa na wanasiasa hao ni kuvunjwa kwa vyama vyote vya siasa nchini humo, kitendo ambacho wamesema kinarudisha nyuma uhuru wa demokrasia na kisiasa nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *