
Nchini Mali, kiongozi wa shirika la kiraia Ménaka, eneo la kaskazini-mashariki mwa nchi inayopakana na Niger, ametekwa nyara Mei 19, 2025. Sidi Barka alitekwa nyara katikati ya jiji na watu wasiojulikana. Uwezekano kadhaa unazingatiwa: ule wa wanajihadi kutoka Dola ya Kiislamu katika Sahel au ule wa majambazi wa ndani wanaofanya vitendo vya uhalifu tu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Alikuwa akitokea msikitini anarudi nyumbani kwa amani kati ya saa 1:30 usiku na saa 2 usiku baada ya sala ya Laisha. Lakini, kulingana na wasaidizi wa Sidi Barka na maafisa wa eneo hilo waliowasiliana na RFI, wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki walikuwa wakimsubiri karibu na nyumbani kwake. Baada ya kumtisha na kumzuia asikimbii kwa kufyatua risasi hewani, wavamizi hao wawili walimchukua kwa nguvu. Vyanzo vingine vinasema kwamba Tasbihi na viatu vyake viliokotwa chini.
Sababu za wakimbizi wa ndani
Kiongozi wa shirika la kiraia la Ménaka, Sidi Barka ni mtu wa ndani anayejulikana na wote. Katika miaka ya hivi majuzi, amekuwa akitetea makumi kwa maelfu ya wakimbizi wa ndani ambao wameondoka katika maeneo ya eneo hilo na kutafuta hifadhi katika mji wa Menaka, wakikimbia ghasia hasa kutoka kwa kundi la Islamic State katika Sahel (IS), lakini pia kutoka kwa jeshi la Mali na washirika wake wa Wagner.
Islamic State? Majambazi wa ndani?
Tawi la Sahel la Islamic State linadhibiti karibu eneo lote, na hivi karibuni lilichukua mateka watu kadhaa katika nchi jirani ya Niger, ambao wanaaminika kushikiliwa katika eneo la Menaka. Njia ya jihadi kwa hivyo inazingatiwa. Kutekwa nyara kwa Sidi Barka kunaweza pia kuwa kazi ya majambazi wa ndani wenye nia chafu kabisa. Kwa wakati huu, hakuna madai au ombi la fidia yamefanywa, lakini utekaji nyara bado ni wa hivi majuzi.
Jeshi la Mali na MSA (Movement for the Salvation of Azawad), kundi llenye silaha linaloshirikiana na vikosi vya kitaifa, wanahamasishwa kwa ajili ya utafutaji huo.