Mali: Baada ya kufutwa kwa vyama, mageuzi yataendelea, ‘upinzani’ unapangwa

Nchini Mali, mamlaka ya mpito inabainisha hatua zinazofuata katika mchakato wa mageuzi. Kufuatia kufutwa kwa katiba ya vyama vya siasa siku ya Jumatatu, Mei 12, na kuvunjwa kwa vyama na mashirika yote ya kisiasa nchini siku iliyofuata, Waziri Mjumbe mweye dhamana ya Mageuzi ya Kisiasa amezungumza na vyombo vya habari vya Mali siku ya Jumatano, Mei 14. Anaahidi mchakato “uliojumuisha”.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wanajiandaa kupinga kufutwa huku mbele ya mahakama na, kwa ujumla zaidi, wanapanga “upinzani” dhidi ya serikali iliyopo.

Mamani Nassiré, ambaye binafsi alitangaza kuvunjwa kwa mashirika ya kisiasa siku ya Jumatatu juma hili, ameelezea kwa kina hatua zinazofuata. Kulingana na matamshi yake, yaliyoripotiwa na Gazeti la serikali la L’Essor, waziri mjumbe anayesimamia Mageuzi ya Kisiasa, kama inavyotarajiwa, alitangaza kuunda sheria mpya ya kuamua masharti ya uundaji na uendeshaji wa vyama vya siasa vya siku zijazo, ambapo idadi ya vyama hivyo italazimika kupunguzwa kwa kiasi kikubwa. Mashauriano yaliyoratibiwa mwezi uliopita na mamlaka ya Mpito yalipendekeza idadi ya vyama kuwa viwili, vitatu au vinne – ikilinganishwa na karibu 300 hivi sasa – pamoja na masharti magumu zaidi ya uundaji wa chama – dhamana kubwa ya kifedha inaweza kuhitajika.

Mchakato “Jumuishi”, bila vyama vya siasa

Mapendekezo mengine ambayo sheria ya baadaye itabidi izingatie ni pamoja na kukomesha uhamaji wa kisiasa – mwanasiasa kuhama kutoka chama kimoja hadi kingine – na kuondoa ufadhili wa umma. Hadhi ya kiongozi wa upinzani inaweza kutoweka, kama ilivyopendekezwa na mashauriano, au kuunganishwa katika hati ya baadaye ya vyama vya siasa, kama ilivyopendekezwa na waziri mjumbe.

Mamani Nassiré ameahidi kuwa mchakato huo utakuwa “jumuishi”: “Tutawaita watu wote wanaoweza kuchangia katika kutunga sheria nzuri kwa mujibu wa Katiba na matarajio ya raia wa Mali,” amesema waziri mjumbe huyo, bila kubainisha alikuwa akimfikiria nani. Vyama vya kwanza vinavyohusika, yaani vyama vya siasa vyenyewe, havitaweza kushiriki, kwa vile havipo tena na shughuli zao sasa zimepigwa marufuku. Kwa vyovyote vile, mapendekezo madhubuti waliyotoa mwezi Machi, kwa nia ya mkataba mpya, yalichukuliwa kuwa hayatoshi na Mamani Nassiré, ambaye amehalalisha kufutwa kwa vyama kwa jukumu lao la kuvuruga utulivu, ambalo alisema lilikuwa na madhara kwa utulivu wa umma.

Kuhakikidha jeshi linabaki madarakani

Haya yote ni maelezo “ya uwongo”, kulingana na viongozi wa kisiasa waliowasiliana na RFI, ambao wanakumbusha kuwa waliwasilisha mapendekezo madhubuti – kupunguza idadi ya vyama, kudhibiti ufadhili, nk – na ambao walichukua uangalifu wa kuheshimu mfumo wa kisheria wakati wa kuelezea madai yao. Viongozi wa vuguvugu la kuunga mkono demokrasia kwa kauli moja wanaamini kuwa lengo pekee la mageuzi hayo ni kuhakikisha kuwa wanajeshi walionyakua madaraka miaka mitano iliyopita wanaweza kusalia madarakani bila kukabiliwa na upinzani. Na bila kufanya uchaguzi, njia ambayo ni rasmi moja ya “mapendekezo muhimu” kutoka kwa “mashauriano ya wadau muhimu” maarufu mwezi uliopita.

Hatua za kisheria za kupinga uvunjaji

Lakini ni njia gani ya kuchukua hatua iliyosalia kwa wanaharakati wanaounga mkono demokrasia sasa? Kuvunjwa kwa vyama vya siasa kunawakataza kuwa na mkutano wowote au kutoa tamko lolote. Mazungumzo rahisi ya simu kati ya viongozi wawili wa vyama yanaweza kuchukuliwa kuwa “shughuli” haramu inayoadhibiwa na sheria.

Viongozi kadhaa wa waandamanaji wametangaza hatua zijazo za kisheria, mbele ya Mahakama ya Kikatiba, Mahakama ya Juu na mamlaka nyingine, kupinga kufutwa kwa vyama hivyo, ambao wanachukulia uamuzi huo kuwa ni “kinyume cha katiba.” Lakini kuanzisha tu hatua hiyo kunaweza kuchukuliwa kuwa kosa kwa vyama vilivyosimamishwa. “Hatua hizi zitachukuliwa kwa niaba ya watu ambao wana kila haki ya kufanya hivyo,” amesema waziri wa zamani.

“Upinzani wajiandaa kupinga kwa njia za kisheria “

“Taarifa inatayarishwa,” mwingine anasema, akiongeza kuwa “muundo na maudhui” bado yanazingatiwa “ili kubaki ndani ya mfumo wa uhalali.” Wakati wanaharakati wanaounga mkono demokrasia kila mara wamekuwa wakitumia mbinu hii kwa uangalifu, kufutwa kwa mashirika ya kisiasa sasa kunawalazimisha katika aina ya usiri.

“Tuna mkutano hivi karibuni, lakini sitaki kukuambia siku kamili kwa sababu za usalama,” mwasiasa mmoja wa upinzani amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *