Malengo ya Iran ya kuwa na ushirikiano mzuri na majirani zake katika nyuga mbalimbali

Majid Takht Ravanchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisiasa amesema kuhusu mikutano na mazungumzo aliyofanya na maafisa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) au Imarati kwamba majirani wana nafasi maalumu katika sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.