Makundi ya kutetea Palestina ya Uingereza: Amani ya kudumu huko Gaza itapatikana kwa kukomesha uvamizi wa Israel

Makundi kadhaa ya wanaharakati wa Kipalestina nchini Uingereza yametoa wito wa kukomeshwa uvamizi wa Israel na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina, baada ya kutangazwa makubaliano ya kuzisitisha vita kati ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na utawala ghasibu wa Israel.