Makumi ya mateka wa Kipalestina waachiliwa huru, Hamas yakabidhi maiti

Makumi ya mateka wa Kipalestina wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mji wa Quds wameachiliwa huru mapema leo Alkhamisi alfajiri ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kubadilishana mateka kati ya Muqawama na Israel, na wamepokewa kwa shangwe kubwa Ramallah.