Makumi wauawa na kujeruhiwa baada ya askari wa Israel kuwafyatulia risasi raia kusini mwa Lebanon

Vikosi vya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel vimewafyatulia risasi raia wa Lebanon wanaorejea makwao katika miji ya kusini mwa nchi hiyo, na kuua watu wasiopungua watatu na kuwajeruhi wengine 44.