Makubaliano ya nyuklia ya Iran: Beijing, Moscow na Tehran yataka kukomeshwa kwa vikwazo

China, Iran na Urusi zimetoa wito siku ya Ijumaa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Tehran wakati wa mazungumzo ya pande tatu mjini Beijing huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka Washington kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Majadiliano haya ya ngazi ya juu yanafanyika katika mji mkuu wa China katikati ya mvutano wa kidiplomasia, huku mataifa makubwa yakitarajia kufufua makubaliano ya kimataifa ya 2015.

Haya yanajiri wakati ambapo Donald Trump, ambaye aliiondoa Marekani kwenye makubaliano hayo mwaka 2018 wakati wa muhula wake wa kwanza, amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na Tehran tangu arejee madarakani.

Lakini wakati huo huo, rais wa Marekani ameimarisha vikwazo dhidi ya Iran, na ananyooshewa kidole cha lawama na viongozi wa Iran.

“Tumefanya mzungumzo ya kina juu ya masuala ya nyuklia na kuondolewa kwa vikwazo,” na “kusisitiza haja ya kukomesha vikwazo vyote haramu vya upande mmoja,” Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu amesema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wenzake wa Urusi na Iran.

Amezungumza baada ya mkutano na wenzake wa Urusi Sergei Ryabkov na Kazem Gharibabadi, waziri wa Iran.

Waatatu hao “wamesisitiza haja ya kukomesha vikwazo vyote visivyo halali vya upande mmoja,” Ma amesema pamoja na manaibu wengine wawili wa mawaziri, akirejea maneno ya taarifa ya pamoja ya China-Urusi-Iran iliyotolewa na Beijing.

Ma Zhaoxu amesema kuwa mkuu wa diplomasia ya China, Wang Yi, atakutana na Ryabkov na Gharibabadi, na kisha watatoa “hotuba muhimu.”

– Gamba tupu –

Nchi za Magharibi zimeishuku Tehran kwa kutaka kupata silaha za nyuklia kwa miongo kadhaa. Iran inakanusha vikali hili na inadai mpango wake upo kwa madhumuni ya kiraia tu, ikiwa ni pamoja na nishati.

Mwaka 2015, Iran ilifikia makubaliano na nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (China, Urusi, Marekani, Ufaransa na Uingereza) na Ujerumani kudhibiti mpango wake wa nyuklia.

Iran ilikuwa ikiheshimu ahadi zake, kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA). Mkataba huo uliipatia nchi hiyo msamaha wa vikwazo kwa kubadilishana na mpango wake wa nyuklia.

Lakini mnamo 2018, Donald Trump aliondoa nchi yake kutoka kwa makubaliano hayo. Vikwazo vya Marekani vilirejeshwa na uchumi wa Iran haukuweza kukuwa tena.

Katika kulipiza kisasi kwa kujiondoa kwa Marekani, Iran nayo iliasi ahadi zake na kuendeleza mpango wake wa nyuklia.

Majaribio yote ya kufufua makubaliano ya 2015, ambayo sasa ni ganda tupu, yameshindwa katika miaka ya hivi karibuni.

Azimio hilo linatumika hadi mwezi Oktoba mwaka huu, na baadhi ya nchi haziondoi haja ya kuiwekea tena vikwazo Tehran baada ya tarehe hiyo.

Iran tayari imefanya duru kadhaa za mazungumzo na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza (E3 group) kuhusu mpango wake wa nyuklia katika miezi ya hivi karibuni.

Mazungumzo ya Ijumaa mjini Beijing yanalenga “kuimarisha mawasiliano na uratibu, kwa nia ya kuanza tena mazungumzo mapema,” Mao Ning, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, alisema siku ya Alhamisi.

– “Kutokuwa na umakini” –

Tangu arejee Ikulu ya Marekani, Donald Trump amesema yuko tayari kwa mazungumzo na Iran kuhusu masuala ya nyuklia. Alifichua kwamba ameandika barua kwa viongozi wa Iran, huku akionya kuhusu uwezekano wa kuchukuliwa hatua za kijeshi ikiwa Tehran itakataa.

“Tishio hili ni la kutoa kuwa na umakini,” Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alijibu siku Jumatano. Alisema Tehran “ina uwezo wa kulipiza kisasi.”

Donald Trump anafuata sera ya kile kinachoitwa “shinikizo la juu” dhidi ya Iran, iliyoanzishwa wakati wa muhula wake wa kwanza (2017-2021), na kuanzishwa tena kwa vikwazo ili kudhoofisha nchi kiuchumi.

Serikali ya Marekani ilitangaza vikwazo vipya siku ya Alhamisi dhidi ya Waziri wa Mafuta wa Iran Mohsen Paknejad, pamoja na mashirika na meli kadhaa zinazotuhumiwa kusaidia nchi hiyo kukwepa vikwazo vya kimataifa dhidi ya mafuta yake ghafi.

Hatua iliyolaaniwa Ijumaa na Tehran, ambayo imeshtumu”unafiki” wa Washington.

Marekani ilikuwa tayari imetangaza mwezi uliopita msururu wa hatua dhidi ya watu binafsi, makampuni na meli zinazotuhumiwa kukwepa vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran.

Mwishoni mwa mwezi wa Februari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi alifuta “mazungumzo ya moja kwa moja” na Marekani katika muktadha wa sasa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *