Makardinali 133 kumchagua Papa mpya

Vatican. Makardinali 133 kuanzia Mei 7, 2025 watashiriki mkutano maalumu kumchagua Papa mpya wa 267 kufuatia kifo cha Papa Francis kilichotokea Aprili 21 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Angella Rwezaula na kuchapishwa na mtandao wa Vatican News, makardinali hao wanatoka nchi 71 katika mabara matano.

Hao ni makardinali wa mataifa 17 ya Afrika, 15 ya  Amerika, 17 Asia, 18 Ulaya na manne Oceania.

Kwa mara ya kwanza, makardinali 15 wapigakura ni wa asilia kutoka upande mmoja wa sayari hadi mwingine ambao ni kutoka Haiti, Cape Verde, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Papua New Guinea, Malaysia, Sweden, Luxembourg, Timor ya Mashariki, Myanmar, Singapore, Paraguay, Sudan Kusini, Serbia, Rwanda na Tonga.

Mpigakura mdogo ni Kardinali wa Australia, Mikola Bychok, mwenye miaka 45 na mwenye umri mkubwa zaidi ni Mhispania Carlos Osoro Sierra, mwenye miaka 79.

Makardinali wengi zaidi ni waliozaliwa mwaka 1947 ambao 13 watapiga kura wakiwa na miaka 78 au wanatarajia kutimiza umri huo.

Ni Kardinali Baldo Reina pekee aliyezaliwa mwaka 1970, ambaye atafikisha miaka 55 Novemba 26, mwaka huu. Makardinali Leo Frank, aliyezaliwa mwaka 1971 na Rolandas Makrickas, aliyezaliwa mwaka 1972, hawana watu wa rika moja.

Wapigakura katika mkutano huo, wapo makardinali watano walioteuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II. Wapo 22 walioteuliwa na Papa Benedict XVI na 108 walioteuliwa na Papa Francis.

Katika kundi la makardinali watawa wa mashirika wapigakura ni 33 kutoka familia 18 za kitawa.

Makardinali wanaunda baraza maalumu ambalo kazi yake ni kuandaa uchaguzi wa Papa wa Roma na humsaidia Papa kwa kufanya kazi pamoja wakati wanaitwa ili kushughulikia mambo muhimu zaidi na kama watu binafsi, katika shughuli mbalimbali zinazofanyika.

Makardinali ambao hawajafikisha umri wa miaka 80 ndio humchagua Papa, hivyo hutofautishwa kati ya makardinali wapigakura na wasio wapigakura.

Baraza hilo kwa sasa linaundwa na makardinali 252, kati yao 135 ni wapigakura na 117 ni wasio wapigakura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *