
Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance amekutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi mjini New Delhi Jumatatu, Aprili 21, maafisa wa serikali ya India wamesema, huku biashara ikitarajiwa kuongoza ajenda ya mazungumzo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na msemaji wa makamu wa rais wa Marekani, Bw. Vance na Bw. Modi watafanya kwanza mkutano wa nchi mbili, kabla ya Bw. Modi kumpokea kwa chakula cha jioni.
Narendra Modi na JD Vance wanatarajiwa kujadili maendeleo yaliyofikiwa kwenye ajenda ya nchi mbili yaliyoanzishwa mwezi mwezi Februari wakati wa mkutano wa kiongozi huyo wa India na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Washington. Ajenda hii inajumuisha “haki” katika biashara kati ya nchi hizi mbili na maendeleo ya ushirikiano wao wa ulinzi.
Mshirika mkubwa zaidi wa biashara
Marekani ndiyo mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa India, huku biashara ya nchi mbili ikitarajiwa kufikia dola bilioni 129 mwaka 2024, na ziada ya dola bilioni 45.7 kwa ajili ya India, kulingana na data ya serikali ya Marekani.
Serikali ya India inatarajia kuchukua fursa ya kusitisha kwa siku 90 kwa Donald Trump kwa kuanzishwa kwa kile kinachojulikana kama ushuru wa kulipiza ili kuhitimisha makubaliano ya biashara. “Tuna matumaini makubwa kwamba ziara hii (ya JD Vance) itatoa msukumo mpya kwa uhusiano wetu wa nchi mbili,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya India Randhir Jaiswal aliwaambia waandishi wa habari siku ya Alhamisi.
Safari ya JD Vance kwenda India pia inaweza kuandaa njia ya ziara ya Donald Trump nchini humo baadaye mwaka huu, wakati wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Quad, ambao unajumuisha India, Australia, Japan na Marekani.
“Ukweli kwamba mvutano kati ya Marekani na China unaongezeka, na kwamba JD Vance hasa anaonekana kuwa na jukumu muhimu sana katika diplomasia ya Marekani, pia inamaanisha kuwa ziara hiyo ina umuhimu zaidi,” anabainisha Harsh Pant, mkurugenzi wa sera za kigeni katika Taasisi ya Utafiti ya Observer huko New Delhi.
Vance ataandamana na maafisa wa utawala wa Marekani, lakini haijafahamika kwamba pande hizo mbili zitatia saini makubaliano yoyote wakati wa ziara hiyo, vyanzo vinavyofahamu suala hilo vimesema.