Makabiliano ya risasi yaripotiwa kati ya jeshi la DRC na waasi wa AFC/M23

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, milio ya silaha nzito na nyepesi ilisikika usiku wa Aprili 11-12 katika mji wa Goma

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, makabiliano hayo makali yalihusishwa na wapiganaji wa Wazalendo na wanajeshi wa jeshi la Kongo ambao walikabiliana kwa risasi na waasi wa AFC-M23 wanaoukalia Mji huo.

Milio ya risasi hii nzito ilianza katika wilaya ya Ndosho kuelekea balindu kabla ya kuenea katika wilaya kadhaa za magharibi mwa jiji jioni ya Aprili 11.

Wakazi wanaelezea kuishi katika hali ya wasiwas kwenye vitongoji kama vile Ndosho, Kyeshero na Mugunga.

Milio ya silaha nzito na nyepesi iliyoambatana na milipuko ya makombora ilisikika pia katika eneo la Ndosho na Mugunnga na viunga vya eneo la Nyiragongo.

“Tulijificha chini ya vitanda kwa sababu ya milio ya risasi. Hatujui ni nini hasa kinaendelea,” wakaazi kadhaa wa eneo hilo waliiambia RFI.

FARDC inapambana na waasi wa M23

Uvamizi huu unakuja wakati mapigano makali yakiripotiwa kwa siku tatu kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, katika eneo la Nyiragongo, karibu na hifadhi ya kitaifa ya Virunga.

Mapigano yameendelea kati ya kundi ambalo linawajumuisha wapiganaji wa Wazalendo, FARDC, FDLR na waasi wa AFC-M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *