Mahathir azikosoa EU, US kwa mauaji ya kimbari Gaza, asema ‘Ustaarabu umefeli’

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia amekosoa vikali uungaji mkono wa Marekani na Umoja wa Ulaya kwa Israel akisisitiza kuwa, kuunga mkono kwa hali na mali mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza ni jambo la ‘kuchukiza na kukirihisha.’