Mahakama ya Marekani yatishia utawala wa Trump kwa kudharau mwenendo wa mahakama

Je, msuguano huu unaozidi kuwa mbaya na kutia wasiwasi kati ya serikali ya Marekani, utawala wa Trump, na mahakama utaipeleka wapi Marekani?  Kwa sababu katika enzi hii ya Trump 2, Ikulu ya White House inachagua kutofuata maamuzi ya mahakama na majaji wawili sasa wanatishia ikiwa utawala wa shirikisho utaendelea kukiuka maamuzi yao kimakusudi.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Majaji wawili wanabaini kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba utawala wa Trump utapatikana na hataia ya kudharau mahakama kwa sababu umeshindwa kuzingatia maamuzi ya kufukuzwa kwa wahamiaji haramu. Huu ni uamuzi wa pili katika muda wa saa 24 unaoshtumu dharau ya utawala wa Trump, au hata imani mbaya, kuhusiana na mahakama zinazozuia sera yake ya kuwafukuza watu wengi.

Jaji Boasberg amebainisha kuwa wakati wa uamuzi wake wa Machi 15, watu waliohusika “walikuwa kwenye ndege zinazoelekea nchi za kigeni baada ya kufukuzwa kutoka Marekani na serikali kabla ya kudai haki zao kwa kupinga kufukuzwa kwao katika mahakama ya shirikisho.” “Badala ya kuzingatia uamuzi wa mahakama, serikali iiliendelea na operesheni yake ya kuwafukuza,” amesema.

“Walipuuza uamuzi wa mahakama kwa makusudi”

Maafisa wa utawala wa Trump “hawajatoa sababu za msingi za kuepuka hitimisho dhahiri kutoka kwa ukweli wa kesi: kwamba walipuuza uamuzi wa mahakama kwa makusudi,” jaji amebainisha. Jaji huyo hata hivyo ameipa serikali hadi Aprili 23 kuepuka kesi za “kuidharau mahakama” kwa kuzingatia uamuzi wake wa awali. Vinginevyo, anaimba serikali kuwasilisha utambulisho wa mtu/watu waliochagua kuipuuzia. Ikulu ya White House imetangaza kuwa itapinga matokeo haya mahakamani.

Majaji wengine wanazuia baadhi ya maagizo ya utendaji ya Donald Trump: kuajiri watumishi wa umma, kutolewa kwa fedha zilizo kusudiwa katika sekta ya Tabianchi na miundombinu ambazo zilizuiliwa kumeagizwa hivi majuzi, anaripoti mwandishi wetu wa New York, Carrie Nooten. Lakini chama cha Republican kinawatuhumu majaji kwa “kunyakua” mamlaka ya ofisi kuu na kudhoofisha sifa zao kwenye mitandao ya kijamii.

Kitu pekee ambacho kinaweza kuushawishi utawala kutii sheria za mahakama ni kama Bune Congress litawajibika, yaani, wabunge wa chama cha Republican, lakini kwa sasa, wanaogopa, au ikiwa raia watahamasisha. Nguvu za kupingana zinafanya kazi tu kwa nia njema, yaani, kufuata kanuni za kikatiba, anasema Anne Deysine, mwanasheria, profesa wa chuo kikuu na mwandishi wa kitabu “Judges Against America”.

Adhabu ya kudharau mahakama kwa mtu binafsi inaweza kuwa kifungo, faini, au zote mbili. Kwa utawala, ni ngumu zaidi, lakini zaidi ya yote, migogoro hii inaonyesha wazi mipaka ya mahakama katika kutekeleza maamuzi yake mbele ya mamlaka ya utendaji ambayo inavunja sheria. Hii ndiyo sababu baadhi ya wachambuzi wanabaini kwamba Marekani iko kwenye hatihati ya mgogoro wa kikatiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *