Mahakama ya Kijeshi ya DRC yatoa hati ya kukamatwa Corneille Nangaa

Mahakama ya Kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Corneille Nangaa, mkuu wa makundi ya waasi wa mashariki mwa nchi hiyo, ikimtuhumu kwa kushindwa kuzuia vitendo vya utesaji chini ya mamlaka yake.