
Mahakama ya Juu ya Marekani siku ya Jumatatu imetoa idhini kwa utawala wa Trump kuwafukuza wahamiaji kwa kuzingatia sheria ya karne ya 18, huku ikiwaruhusu kupinga uamuzi huo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mahakama ya Juu ya Marekani Jumatatu, Aprili 7, imeidhinisha kufukuzwa kwa wahamiaji chini ya sheria ya karne ya 18, lakini iliwapa “fursa ya kupinga kufukuzwa kwao.”
Rais Donald Trump alitumia sheria hii ya kipekee ya mwaka 1798 – ambayo hapo awali ilitumika tu wakati wa vita – katikati ya mwezi Machi kuwafukuza zaidi ya watu 200 kwenda El Salvador, ambao waliwasilishwa kama washukiwa wa genge.
Donald Trump amepongeza kama “siku kuu ya haki,” licha ya ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu.
Jaji wa serikali hatimaye alizuia kufukuzwa kwa wahamiaji kwa siku 14 kulingana na sheria hii na akaelezea wasiwasi wake kuhusu “tatizo kubwa” za kutumia “Sheria ya Maadui Wageni.”
Donald Trump aliwashutumu watu waliofukuzwa nchini El Salvador bila kufunguliwa mashtaka katikati ya mwezi Machi kuwa ni wa genge la Tren de Aragua.