Magenge yenye silaha yauwa watu 30 katika muda wa siku 3 huko Benue, Nigeria

Watu wasiopungua 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi ya magenge yenye silaha yaliyojiri kwa muda wa siku tatu dhidi ya wakulima jamii mbalimbali katika jimbo la Benue kaskazini kati nchini Nigeria.

Justine Shaku afisa wa serikali za mitaa katika eneo la Katrina Ala katika jimbo la Benue ameeleza kuwa mamia ya watu waliokuwa na silaha jana waliwavamia raia katika jimbo hilo na kuanza kuwafyatulia risasi wakulima na wakazi wa eneo la Katrina Ala huko Benue. 

Afisa huyo wa serikali za mitaa ameeleza kuwa watu wasiopungua 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika hujuma hiyo ya magenge yenye silaha iliyoanza tangu Jumamosi. 

Amesema wahuni hao waliokuwa na silaha waliwashambulia raia katika mashamba na nyumba zao na kisha kuanza kuwafyatulia risasi watu.” Watu hao wenye silaha wanashukiwa kuwa ni kutoka nje ya Nigeria.