Magaidi 70 wa Al Shabab wameuawa nchini Somalia

Somalia inasema maafisa wake wa jeshi wamewauwa magaidi zaidi ya 70 wa Al Shabab, wakati wa opresheni iliyofanyika siku ya Jumanne katika eneo la Hirshabelle, eneo la Kusini na Kati ya nchi hiyo.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Habari inasema operesheni hiyo ilishirikisha vikosi vya serikali na wapiganaji wanaojitolea na kusababihsha mauaji makubwa ya magaidi wa Al Shabab.

Mbali na mauaji hayo, silaha na magari yaliyokuwa yanatumiwa na magaidI hayo yameharibiwa.

Operesheni hiyo imekuja baada ya magaid hao kuripotiwa kutekeleza mashambulio katika eneo hilo kwa kurusha mabamo na kuwashambulia raia katika eneo la Hirshabelle.

Kwa miaka 15 sasa serikali ya Somalia imetangaza vita dhidi ya Al Shabab, kwa msaada wa mataifa ya Afrika, imekuwa ikipambana na Al Shabab, kundi linalolenga kuanzisha uongozi wao katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika.