Magaidi 11 wenye mfungamano na Israel waangamizwa na kutiwa nguvuni mashariki ya Iran

Msemaji wa mazoezi ya kijeshi ya “Mashahidi wa Usalama” katika Kamandi ya Quds ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametangaza magaidi saba wameangamizwa na wengine saba wametiwa mbaroni kwa kuhusika na hujuma za kigaidi mkoani Sistan na Baluchistan, kusini mashariki mwa Iran.

Jenerali Ahmed Shafaei, msemaji wa Manuva ya Mashahidi wa Usalama katika Kamandi ya Quds ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: katika mazoezi ya kijeshi ya Operesheni ya Mashahidi wa Usalama ndani ya kipindi cha saa 48 zilizopita, magaidi mamluki wanne wenye mafungamano na utawala wa Kizayuni wameangamizwa, saba wametiwa mbaroni na watano wengine wamejisalimisha kwa vikosi vya usalama.

Kwa mujibu wa msemaji wa Mazoezi ya Operesheni ya Mashahidi wa Usalama katika Kamandi ya Quds ya Jeshi la Nchi Kavu la IRGC, mazoezi hayo yanaendelea kufanyika kwa lengo la kuimarisha na kuupa uimara usalama endelevu; na makamanda na askari wa Kamandi ya Quds ya Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wataendelea na oparesheni zao hizo kwa azma thabiti hadi kufikia kikamilifu malengo ya mazoezi hayo…/