Mafuriko nchini Australia yamesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 50,000 wamenaswa

Australia Mashariki inakabiliwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa. Mwanamume mmoja amepatikana amekufa katika nyumba iliyojaa maji na watu wapatao 50,000 wamenaswa siku ya Alhamisi na hawana msaada wowote.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Australia kwa mara nyingine tena inakabiliwa na mafuriko kutokana na mvua zinazonyesha. Mvua kubwa iliyonyesha mashariki mwa nchi hiyo imenasa watu 50,000 na kumuua mkazi mmoja, Waziri Mkuu wa New South Wales Chris Minns ametangaza Alhamisi, Mei 22.

Polisi wameupata mwili wa mzee wa miaka 63 katika nyumba iliyojaa maji katika kitongoji cha Moto, takriban kilomita 400 kaskazini mashariki mwa Sydney.

“Lazima niseme pia kwamba tunajitayarisha kwa habari mbaya zaidi katika saa 24 zijazo. Maafa haya ya asili yamekuwa mabaya kwa jumuiya hii,” amesema Chris Minns.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *