Mafanikio ya NIDA katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita

Tunapo zungumzia mafani­kio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inapofik­isha kipindi cha miaka 4 mada­rakani, huwezi kuacha kuzun­gumzia mafanikio makubwa ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambayo ndiyo taasisi yenye dhamana ya usaji­li na utambuzi wa watu nchini.

Katika kipindi hicho NIDA imeendelea kuimarisha na kutekeleza shughuli za usajili na utambuzi wa watu nchini kote Tanzania Bara na Zanzi­bar kupitia ofisi za usajili za wilaya ili kuhakikisha watu wote wenye vigezo wanasajili­wa na kutambuliwa.

Jumla ya wananchi 3,581,830 wamesajiliwa na kutambu­liwa katika kipindi hicho hivyo, kufikisha jumla ya wananchi 25,634,890 waliosajiliwa na kutambuliwa toka kuanza kwa usajaili na utambuzi wa watu mwaka 2012, sawa na asilimia 81.4 ya watu 31,477,938 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kaji.

Mafanikio ya usajili yanato­kana na Serikali kuiwezesha NIDA kusogeza huduma za usajili na utambuzi karibu na makazi ya watu kwa kuanzisha Ofisi za Usajili za Wilaya na vituo vya usajili 142 Tanzania Bara na 11 Zanzibar.

Vivyo hivyo katika kipindi hicho cha miaka minne, takrib­an Namba za Utambulisho wa Taifa (NINs) 2,656,801 zimeza­lishwa hadi kufikia Februari 2025 na hivyo kufanya namba zilizokwisha kutolewa kuwa 21,426,716 sawa na asilimia 83.6 ya watu waliosajiliwa.

Katika kuondokana na tatizo la upatikanaji wa vitambulisho kwa wananchi, NIDA ilikuja na mpango mkakati wa uzalish­aji mkubwa wa vitambulisho vya Taifa (Mass production) sambamba na ugawaji wa vit­ambulisho kwa umma (mass issuance) ulioaza kutekelezwa Oktoba 2023.

Msemaji wa NIDA, Geofrey Tengeneza amesema uzalishaji huo mkubwa ni matokeo ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuiwezesha NIDA kupata fed­ha kwa ajili ya kulipa deni la mkandarasi wa kadi ghafi la Sh 17,578,313,987.78 na fedha za kununua kadighafi 13,516,593 kiasi cha Sh 42,500,000,000.00 na kuweza kufanikisha kununua kadighafi 13,735,728 na kazi ya uzalishaji vitambulisho ikaanza kwa kasi kubwa na hadi Machi, 2024 wananchi wote waliosajiliwa na kupatiwa Namba za Utambulisho (NINs) vitambulisho vyote vilikuwa vimekwishazalishwa.

Amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi, 2021 hadi kufikia Februari, 2025 jumla ya vitambulisho 14,987,162 vimezalishwa kwa wananchi. Idadi hii inafanya jumla ya vitambulisho vya Taifa vilivyokwisha kuzalishwa kufikia 21,270,895. Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Has­san imeiwezesha NIDA kum­aliza tatizo la muda mrefu la upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi.

Aidha jumla ya vitambulisho 13,423,497 vimesambazwa na kugawiwa kwa wananchi katika kipindi hicho cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita na kufanya jumla ya vitambulisho vilivyosambazwa na kugawiwa kwa wananchi kufikia 21,146,582 tangu kuanza kwa usajili mwaka 2012.

Mafanikio ya ugawaji yame­tokana na jitihada za Serikali kupitia NIDA zikiwemo za kuanza kutuma ujumbe mfupi wa ujumbe mfupi (SMS) ili kuwataarifu wananchi kwenda katika ofisi za wilaya kuchukua vitambulisho vyao.

Kuhusu usajili wa Watanza­nia waishio nje ya nchi (Dias­pora), NIDA imeanza kutoa huduma za usajili na utambuzi kwa Watanzania waishio nje ya nchi. Watanzania 500 walipati­wa Namba za Utambulisho na vitambulisho vya Taifa.

Aidha, mfumo wa utam­bulsho wa Taifa unatumika katika kudhibiti mipaka kwa kuhakikisha kuwa watu wote wanaoingia au kutoka ndani ya nchi wanatambulika kwa usa­hihi.

Katika kipindi hicho, NIDA imefanikiwa kuunganisha ofisi zake za usajili za wilaya 22 na kituo cha uchakataji wa taar­ifa na kufanya ofisi za usajili zilizounganishwa kufikia 153. Lengo ni kuwezesha mawasilia­no kati ya ofisi za usajili na kuhakikisha maombi ya watu wote waliosajiliwa yanasa­firishwa kwa haraka kwa njia ya mtandao kutoka Ofisi za Usajili za Wilaya kwenda Kituo cha Kuchakata Taarifa kwa ajili ya uchakataji na uzalishaji vit­ambulisho kwa wakati.

Eneo jingine ambalo NIDA imefanikiwa ni kuwawezasha wananchi kujisajili kwa njia ya mtandao. NIDA imefanikiwa kuunda mfumo unaowaweze­sha wananchi kujisajili katika hatua za awali kwa kujaza taar­ifa zao binafsi wakiwa katika maeneo yao au popote kwa njia ya mtandao (online registra­tion) ili kuwapunguzia muda wa kuhudumiwa kwenye Ofisi za Usajili za Wilaya

Mafanikio mengine ya kuji­vumia kwa NIDA ni kuwe­za kukusanya takriban Sh 126,376,793,030.14 kwa kipindi cha kuanzia Machi, 2021 hadi Februari, 2025 na hivyo, kuon­geza wigo wa makusanyo ya fedha za Serikali. Mafanikio haya yanayotokana na NIDA kuwa na Kanzidata yenye taar­ifa za watu. Aidha, fedha hizo zimewasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

“Kufuatia mafanikio hayo ya ukusanyaji, mwaka 2023 NIDA ilitunukiwa na Mhe Rais tuzo ya mshindi wa tatu miongoni mwa taasisi na mashirika ya Serikali yasiyo ya kibiashara yaliofanya vizuri zaidi katika kuchangia Mfuko Mkuu wa Serikali” amesema Tengeneza.

Aidha, NIDA imefanikiwa kuboresha utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii nchini kwa kuunganisha taasisi za Serikali na binafsi katika Rejes­ta ya Taifa ya Usajili na Utam­buzi wa watu kupitia mfumo wa maunganisho (Common Interface Gateway -CIG) ulio­jengwa na kusanifiwa na wata­alamu wa NIDA.

Mfumo huo unaziwezesha taasisi kupata taarifa binafsi za watu ambazo zimeshaku­sanywa na NIDA kutoka kwe­nye Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi badala ya kuziku­sanya tena. Taarifa hizo zina­tumika kuhakiki na kupunguza au kuondoa vihatarishi vya kughushiwa kwa taarifa binafsi wakati wa kupokea huduma.

Jumla ya taasisi 124 (59 za Serikali na 65 za binafsi) zimeunganishwa na Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utam­buzi. Taasisi hizo zinajumuisha taasisi za sekta ya afya, elimu, kilimo, mawasiliano, mifuko ya hifadhi ya jamii, kodi, ucha­guzi na ardhi. Kuunganishwa kwa taasisi hizo kumeweze­sha maendeleo katika huduma nyingi kama vile;

Usimamizi wa rasilimali watu

Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa watu imeun­ganishwa na mfumo wa Sek­retarieti ya Ajira ili kuweze­sha utambuzi wa watu wote wanaoomba ajira katika utu­mishi wa umma na kuwabaini watu wenye vigezo vya kupata ajira ikiwemo umri na uraia wa mtu. Aidha, rejesta imeweze­sha kuondoa watumishi hewa, kupunguza ajira kwa watoto kwa kuhakiki umri wa mwom­baji wa ajira.

Huduma jumuishi za kifedha

Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa watu imeweze­sha kufanikisha utekelezaji wa sera ya mfumo wa fedha jumuishi nchini kwa kuwapa­tia wananchi, hasa kwa vijana na wanawake utambulisho wa kipekee (legal identity) ambao ni msingi wa kuwawezesha kupata huduma katika taasisi za fedha.

Hivyo, wananchi waliokuwa wanakosa huduma za Kibenki kwa kukosa nyaraka rasmi zin­azowatambulisha wanaweza kupata huduma hizo kwa kutu­mia kitambulisho cha Taifa.

Aidha, Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa watuni nyenzo muhimu ya utekelezaji wa Sera ya Mfahamu Mteja Wako inayosaidia watoa huduma za kifedha kuwaju­muisha na kuthibitisha taarifa za wateja kwa ufanisi na kwa wakati.

Ofisa wa NIDA (kushoto) akitoa huduma ya uandikishaji wa kitambulisho cha Taifa kwa mwananchi.

Hivyo, wateja wote wa mabenki wanatumia Namba ya Utambulisho wa Taifa katika kufungua akaunti na kuomba mikopo ambapo imeongeza ufanisi katika kutoa huduma mathalani kwa sasa wanan­chi wanafunguliwa akaunti za benki papo hapo kwa kutumia namba/kitambulisho cha Taifa.

Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa watu inaweze­sha taasisi za fedha kutumia muda mfupi katika kufanya uhakiki wa taarifa za waom­baji na kutoa huduma au miko­po kwa watu sahihi na hivyo kufanya taasisi hizo kupun­guza masharti magumu katika utoaji wa mikopo.

Hali hiyo, inapunguza ghara­ma za mikopo (riba) pamoja na kuongeza ukuaji wa sekta ya fedha jumuishi. Pia, inaweze­sha kupunguza gharama za uendeshaji na vihatarishi kati­ka taasisi za fedha. Hayo yote yanachangia kasi ya ukuaji wa uchumi katika nchi.

Mapato ya Serikali

Rejesta inatumika katika kusajili namba ya mlipa kodi (TIN) ili kuwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwatambua walipakodi.

Usa­jili wa TIN kwa kutumia Rejesta ya Tai­fa ya Usajili na Utambuzi wa watu kumeongeza usimamizi wa mapato ya Serikali kwa kupata taarifa sahihi za mlipa kodi. Vilevile, rejesta umeun­ganishwa na TRA ili kuweze­sha usimamizi na utambuzi wa uwezo wa walipa kodi kwa kuwa rejesta hiyo inahusisha watu wote ambao wapo katika sekta rasmi na zisizo rasmi hivyo kutambua biashara au uwezo wa mlipa kodi kunapun­guza ukwepaji wa kodi nchini.

Vilevile, maunganisho ya Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa Watuna mifumo mingine yenye taarifa za mali au mapato ya watu kama vile taarifa za ardhi, rejista za magari, taarifa za forodha na rejista za manufaa ya kijamii zinazoweza kutambua biasha­ra au uwezo wa mlipa kodi na hivyo kupunguza ukwepaji wa kodi nchini.

Huduma za afya

Rejesta imeunganishwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kuwezesha wananchi kutambuliwa na kupata huduma za bima ya afya kupitia NHIF. Pia, utekelezaji wa Sera ya Bima ya Afya kwa Wote unatarajia kutumia kit­ambulisho cha Taifa katika kuwatambua wanachama.

Serikali imedhamiria kutu­mia kitambulisho cha Taifa kama kadi ya Bima ya Afya ili kuhakisha uwekezaji wa Seri­kali uliofanyika NIDA unatu­mika katika taasisi nyingine. Mfano, kwa sasa wanafunzi wa elimu ya juu wanatumia Kit­ambulisho cha Taifa kama Kadi ya Bima ya Afya katika kupata huduma za afya nchini. Hii imewezesha Serikali kupungu­za gharama za kuzalisha kadi za bima kwa wanafunzi hao, pamoja na kuhakikisha kuwa huduma husika inatolewa kwa mtu sahihi.

Sekta ya elimu

Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa Watu inawezesha usimamizi na udahili wa wana­funzi wa taasisi za elimu ya juu na kati nchini. Kupitia rejesta hiyo, taasisi za elimu nchini ikiwemo vyuo vikuu vinawe­za kutambua uraia na taarifa zingine za wanafunzi. Aidha, rejesta hiyo imeunganishwa na mifumo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Tanzania (HESLB) na kurahi­sisha mchakato wa udahili wa wanafunzi wanaopaswa kupa­ta mikopo na urejeshaji wa mikopo kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo katika sekta rasmi na zisizo rasmi ndani na nje ya nchi

Maendeleo ya jamii

Rejesta inawezesha Mfu­ko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kutambua wanu­faika ili kuhakikisha misaada inakwenda kwa walengwa. Aidha, rejsta imewezesha TASAF kusajili na kuhakiki wanufaika zaidi ya 376,933 katika kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki hivyo kupun­guza gharama za uendeshaji wa Mfuko pamoja na kuhakiki­sha kuwa wanaopata huduma za mfuko ni walengwa hususan wanawake ambao ndio wanu­faika wakubwa.

Mifuko ya hifadhi ya jamii

Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa Watu inaweze­sha mifuko ya hifadhi ya jamii (PSSSF na NSSF) kutambua wachangiaji na wanufaika wa mifuko na kupunguza udan­ganyifu wakati wa ulipaji wa mafao. Vilevile, Rejesta ina­ongeza ufanisi zaidi kwenye kufanya uhakiki wa wana­chama.

Uwezeshaji wa biashara

Rejesta imeunganishwa na BRELA, BPRA, DSE na TIC ili kuwezesha usajili wa makam­puni ya uwekezaji na biashara nchini. Vilevile, inatumika kuhakiki taarifa za waom­baji wa leseni mbalimbali za biashara kupitia mamlaka ziki­wemo halmashauri.

Mikakati ya nida katika siku zijazo

Akizungumzia baadhi ya mikakati ya Mamlaka, Mkuru­genzi Mkuu wa NIDA James Kaji amesema katika miaka minne mamlaka imefanya maboresho makubwa katika mchakato wa upatikanaji wa vitambulisho na imefanikiwa kurahisisha huduma kwa wananchi.

Kaji amesema, mafanikio yote haya ya NIDA ni juhudi za Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambazo zitasaidia wananchi kiuchumi, kijamii, kiusalama lakini pia na Serikali kupata walipa kodi kwa urahisi.

Kuhusu mikakati ya siku za usoni ya Serikali ya awamu ya sita kupitia NIDA katika kuboresha huduma za usa­jili na utambuzi kwa wananchi. James Kaji amesema kwamba Serikali inayo mikakati mingi ya kuboresha zaidi huduma za usajili na utambuzi. Baadhi ya mikakati hiyo ni kama ifuatayo:

Jamii namba

Kuhusu matumizi ya Jamii Namba kama ilivyoelekezwa na Mheshimiwa Rais, Mkuru­genzi Mkuu huyo amesema NIDA imeanza matayarisho ya usajili wa watoto kuanzia umri wa kuzaliwa ili kuhakikisha suala la utambuzi wa mtu lin­aanza pale anapozaliwa.

Matayarisho hayo ni pamo­ja na mabadiliko ya sheria, utayarishaji wa mifumo ya TEHAMA na ununuzi wa vifaa vitakavyotumiwa na mifumo hiyo. Katika usajili huo taarifa za mtoto zitaunganishwa na taarifa za mzazi au mlezi kati­ka mfumo wa usajili. Jumla ya watoto 30,263,182 wanatara­jiwa kusajiliwa kwa kuzingatia Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Usajili huu utasaidia taarifa za watoto wanapozaliwa kuin­gizwa katika Rejesta ya Taifa ya Usajili na Utambuzi wa Watu na kuendelea kupatika­na kwenye rejesta hiyo katika kipindi chote cha maisha yake duniani.

Utaratibu wa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS)

Kaji amesema kipindi cha nyuma, kabla ya kuamua kuku­sanya vitambulisho vya taifa vilivyokuwa katika kata, vijiji, mitaa na vitongoji walikumba­na na changamoto nyingi.

“Nilipofika hapa tulikubali­ana na wenzangu katika Menejimenti kukusanya vit­ambulisho vyote na kuvipeleka katika ofisi za wilaya, na kuvi­somesha katika Rejesta” ame­sema Kaji.

Amedai kusomesha vit­ambulisho katika rejesta na kwa kushirikiana na mfumo wa TCRA inasaidia katika kutuma ujumbe mfupi wa meseji (sms) moja kwa moja kwa mwanan­chi kupitia simu yake ya mko­noni, kwa kutumia namba ya simu yake anayoitumia hivi sasa bila kujali namba ya usajili iliyotumika awali.

Ameongeza kuwa kuanzia sasa mwananchi yeyote baada ya kuwa amekamilisha usajili wake wa Utambulisho wa taifa na Kitambulisho chake kuchap­ishwa, atapokea ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kumjuli­sha kuwa kitambulisho chake kiko tayari hivyo aende aka­chukue Kitambulisho chake.

Mfumo wa kufahamu hatua za maombi ya utambulisho

Mkurugenzi Mkuu huyo amebainisha kuwa NIDA, ina­tarajia kuzindua mfumo mpya ambao utawaruhusu wanan­chi baada ya kuwa wamejisa­jili hawatalazimika kufuatilia Namba ya Utambulisho wa Taifa katika ofisi za NIDA.

Ni kwamba mwombaji anapokuwa amejisajili ndani ya siku saba, kama maombi ya mwombaji hayana matatizo yeyote mfumo huo utamtumia Namba ya NIDA moja kwa moja kwenye namba yake ya simu ya mkononi, na ndani ya siku 14 anapata Kitambulisho chake, amesema Kaji.

Ofisa wa NIDA akihakiki fomu za wananchi waliojiandikisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vya Taifa.

Amedokeza pia kuwa NIDA inatengeneza mfumo ambao utamwezesha mwananchi kupata ujumbe mfupi sms) kumjulisha hatua ambayo maombi yake yamefikia hadi kitambulisho chache kukami­lika.

“Hii itasaidia sana wanan­chi kwani itapunguza usum­bufu wa kwenda mara kwa mara kufuatilia kitambulisho kwenye ofisi za NIDA au kujua maombi yake yamefikia hatua gani.

Kuongeza thamani ya kit­ambulisho

Mkurugenzi Mkuu wa NIDA James Kaji amesema kwamba Mamlaka hiyo ina mkakati wa kukiwezesha Kitambulisho cha taifa kubeba utambulisho mwingine kama vile Bima ya Afya, lesseni ya gari, cheti cha kuzalia, TIN namba nk. Kutaku­wa pia sehemu ya mengineyo ambako kutawekwa taarifa za kundi la damu la mhusika na taarifa nyinginezo muhimu. Hii itasaidia pale mtu akipata changamoto yoyote, itakuwa rahisi kusaidiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *