Maelfu ya watu wanatarajiwa kuanza kuuaga mwili wa Papa Francis

Mwili wa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, utapelekwa kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, ambako maelfu ya watu wanatarajiwa kuanza kuuaga kwa siku tatu kuanzia siku ya Jumatano, kabla ya kuzikwa siku ya Jumamosi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Viongozi mbalimbali wa dunia, akiwemo rais Donald Trump wa Marekani, watahudhuria mazishi hayo.

Kwa mujibu wa Vatican, ibada yake ya mazishi inatarajiwa kuvutia mamilioni ya raia kutoka kila kona ya dunia na itafanyika katika uwanja wa kanisa la Mtakatifu Peter Basilica, kabla ya kupelekwa kwenye kanisa la Santa Maria Maggiore, ambako alitaka azikwe.

Tayari viongozi kadhaa wa dunia wamethibitisha kushiriki mazishi yake, akiwemo rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky.

Viongozi mbalimbali wa dunia, akiwemo rais Donald Trump wa Marekani, watahudhuria mazishi ya Papa.
Viongozi mbalimbali wa dunia, akiwemo rais Donald Trump wa Marekani, watahudhuria mazishi ya Papa. via REUTERS – Francesco Sforza

Wengine ni waziri mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, mfalme wa wa Uhispania Felipe wa 6 na Malkia Letizia, wengine ni mkuu wa kamisheni ya umoja wa Ulaya, Ursula von Der Leyen.

Hata hivyo rais wa Urusi, Vladmir Putin ambaye wakati mmoja alikutana na papa Francis aliyemsihi akomeseh vita nchini Ukraine, hatahudhuria mazishi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *