Madina, Vicky mguu sawa Sauzi

MADINA Idd na Vicky Elias wamedai zoezi ya kuzisoma changamoto za viwanja vya Leopards Creek, Mpumalanga, Afrika Kusini linaendelea vyema kabla ya michuano ya gofu ya wanawake wa Afrika  kuanza rasmi kuesho kutwa katika viwanja hivyo.

Madina kutoka klabu ya Arusha Gymkhana na Vicky Elias  kutoka Dar Gymkhana ndiyo Watanzania pekee katika michuano hii inaoshirikiua magwiji wa gofu ya wanawsake kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Kwa mujibu wa Madina, Watanzania hawa watashiriki katika maozezi ya kuvifahamu  viwanja siku leo Jumatatu na kesho Jumanne kabla muchuano ya mashino 54 kuanza rasmi siku ya Jumatano,

Yakijulikana rasmi kama African Women Invitational Golf, mashindano yataanza kutimua nyasi katika viwanja kuwa Leopard Creek Country course vilivyoko katika mji wa Mpulanga, nchini Afrika ya Kusini.

“Tutafanza mazoezi siku za Jumatatu na Jumanne kabla kushiriki michuano ya mashimo 18 ya kwanza siku ya Jumatano.  Tutacheza mashimo 18 ya pili siku ya Alhamisi kabla ya kupiga mashimo 18 ya mwisho siku ya Ijumaa ili kukamilisha jumla ya mashimo 54 ya michuanoi hii ya siku tatu,” alisema Madina.

Timu hii ya wacheza gofu wawili iliondoka jana tarehe 2 Februari 2  mwaka huu kwa ajili ya kupata siku mbili za kuvifanyia mazoezi  viwanja wa Leopard Creek.

Madina na Vicky walikuwa na msimu bora mwaka 2024 baada ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa nje ya nchi.

Madina aliuanza msimu uliopita kwa kushinda mashindano ya wazi  ya wanawake nchini Ghana, baadaye kushinda mashindano mawili ya wazi nchini Uganda kabla ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya ubingwa wa Afrika nzima katika mji wa Agadir, Morocco mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa Vicky Elias, mashindano bora kwake yalikuwa ni mchuano wa viwanja vitano vya gofu vilivyoko katika Pwani ya Kenya katika miji ya Mombasa, Kilifi na Malindi ambako alibuka mshindi wa tatu akiwa nyuma ya Mercy Manchma na Mtanzania mwenzake Neema Olomi.

“Tumejianda vyema na hatutawaanguisha Watanzania nchini Afrika Kusini,” alisema Madina Idd.