Madai yasiyo na msingi ya Trump na sisitizo lake la kuendeleza sera ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran

Akirejelea siasa zake za mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena amedai kuwa, siasa hizo zinalenga kuleta amani na kwamba Washington haitairuhusu Iran na nchi nyingine kupata silaha za nyuklia.